1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MINSK. Kiongozi wa upinzani akamatwa

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoH

Kiongozi wa upinzani nchini Belarus Alexander Milinkevinch amekamatwa tena.

Msemaji wake ameeleza kuwa bwana Milinkevinch alikamatwa na maafisa wa ulinzi wa mipaka mara tu baada ya kurejea kutoka Latvia ambako alihudhuria mkutano wa nchi za jumuiya ya kijeshi ya NATO.

Maafisa hao wamedai kuwa mwanasiasa huyo alikuwa na hati bandia.

Msemaji wake pia amefahamisha kuwa bwana Milinkevinch alikutana na rais George Bush wa Marekani ambapo alihakikishiwa mshikamano na rais huyo.

Kiongozi huyo wa upinzani ameshakamatwa mara kadhaa na maafisa wa usalama wa nchi yake Belarus.