Minsk. Ahmedinejad yuko ziarani Belarus. | Habari za Ulimwengu | DW | 21.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Minsk. Ahmedinejad yuko ziarani Belarus.

Rais Alexander Lukashenko wa Belaruss amemuahidi rais mwenzake wa Iran Mahmoud Ahmedinejad kuwa nchi hizo mbili zitashirikiana katika nyanja zote.

Kiongozi huyo wa Iran yuko katika jimbo hilo la zamani la Urusi kwa ziara ya siku mbili.

Wakati wa ziara yake viongozi hao wawili wanatarajiwa kujadili kuhusu nishati, biashara na masuala ya teknolojia.

Lukashenko amekuwa muungaji mkono mkuu wa mpango wenye utata wa kinyuklia wa Iran, wakati Ahmedinejad amemsifu rais huyo wa Belaruss, ambaye anashutumiwa na Marekani kuwa ni dikteta wa mwisho katika bara la Ulaya.

Belarus imekuwa ikihitaji washirika wapya wa kibiashara kutoka nje kwasababu ya hali mbaya ya uhusiano na mshirika wake mkuu wa kiuchumi Russia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com