1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Michuano ya kuania ubingwa barani Ulaya yashika kasi

Nyasi za viwanja mbali mbali vya soka barani Ulaya vimetimka vumbi jana usiku wakati michuano ya champions league ilipokuwa ikiendelea.

default

Michuano ya UEFA

Bayern Munchen waliendelea kubakia katika kundi la A baada ya kutoka sare na Napoli walipochuana San Paolo pale Tony Kroos alipolifunga bao la ushindi. Hata hivyo, Bayern München bado wamewapiku kwa pointi mbili, mahasimu wao ,Italia wanaoongoza kwenye kundi hilo. Timu hiyo ya Ujerumani bado inasubiri kushiriki katika mechi mbili nyengine kati ya tatu zilizosalia wakiwa nyumbani.

Kwa mujibu wa Kocha wa Bayern München, Juup Heynckes, timu yake ilijitahidi.

SSC Neapel vs. Bayern München Flash-Galerie

Mchezaji wa Bayern Munich, Mario Gomez (kulia) wakati wa michuano ya kundi la A kati yao na Napoli.

Kwa upande wake, kocha wa Napoli, Walter Mazzarri, alisisitiza kuwa jambo la msingi ni kuwa wamerejea katika mashindano ya mabingwa barani Ulaya baada ya miaka 21 na kilichosalia ni kujitahidi.

Alex Ferguson

Alex Ferguson, kocha wa Man U.

Kauli ya Sir Alex Fergusson

Wakati huohuo, Manchester United iliifunga timu ya Romania mabao 2-0 katika mechi nyengine ya michuano ya Jumanne. Wayne Rooney wa Man U ndiye aliyepambana na Otelu Galati wa Romania ili kuufanikisha ushindi huo. Katika dakika ya 64, Wayne Rooney aliucharaza mkwaju wa penanti wakati ambapo Nemanja Vidic alilazimika kupambana na Gabriel Giurgiu kwenye dakika mbili zilizofuatia. Mchezaji huyo alifunga bao jenginge kwa penanti nyengine wakati wa majeruhi. Hii ni mara ya kwanza Manchester United inapata ushindi katika timu za kundi la C. Kocha wa Manchester United ,Sir Alex Fergusson, ana mtazamo tofauti ukizizingatia mechi zijazo za kesho.

Kulingana na mtaalam huyo wachezaji wake hawana jinsi ila kujitahidi hata baada ya kuwa na ratiba ngumu tangu mwishoni mwa wiki iliyopita. Timu hiyo kwa sasa imesogea hadi nafasi ya pili ikiwa ni karibu na timu ya Benfica ya Ureno.

Lyon yang'ara

Kwa upande mwengine, Real Madrid iliicharaza Lyon mabao manne kwa bila baada ya Karim Benzema, Sami Khedira, Mesut Oezil na Sergio Ramos kufunga mabao hayo.

Kwengineko, timu za Dinamo Zagreb na Basel zote zilifungwa mabao 2-0 na timu za Ajax na Benfica.

CSKA Moscow nayo iliifunga Trazonspor mabao matatu kwa bila.

Europa League Villareal gegen Leverkusen Flash-Galerie

Giuseppe Rossi wa Villareal (kati) wakati wa mechi yao na Leverkusen.

Benfica haijafungwa katika msimu huu

Mabao yaliyofungwa na Bruno Cesar na Oscar Cardozo yaliipa timu ya Benfica ushindi ilipopambana na Basel nyumbani kwao. Timu hiyo ya Benfica ya Ureno haijafungwa mabao yoyote katika msimu huu. Kufuatia matokeo hayo, kocha wa muda wa timu ya Basel alipata pigo ikiwa ni mechi yake ya kwanza iliyochezwa nyumbani.

Manchester City nayo iliifunga Villareal mabao 2-1 katika dakika ya mwisho alipofunga bao Sergio Aguero. Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini, anasisitiza kuwa lazima wachezaji wake wajifunze zaidi kwani ushindani ni mkubwa.

Roberto Mancini aliendelea kueleza kuwa timu yake inaweza kuingia katika awamu ya pili ikijitahidi.

Fans von Manchester City

Wapambe wa Manchester City

Ushirikiano ndilo la msingi

Inter Milan nayo ilisogea hadi juu katika kundi la timu za B ilipoifunga Lille bao 1-0. Giampaolo Pazzini ndiye aliyelifunga bao hilo la pekee mnamo dakika ya 22. Wesley Sneijder aliyerejea hivi karibu baada ya kujeruhiwa pajani, alikuwa na mchango muhimu kabla ya bao hilo kufungwa.


Wesley Sneijder anausisitizia umuhimu wa kushirikiana ili timu yao ifanikiwe katika msimu huu. Leo hii mechi za timu zilizomo kwenye makundi ya E, F, na G zitachezwa kote barani Ulaya zikiwemo Leverkusen itakayopambana na Valencia, Olympiacos na Dortmund pamoja na Arsenal na Marseille.

Mwandishi: Mwadzaya, Thelma- APE/RTRE/ Uefa.com multimedia.

,

 • Tarehe 19.10.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/12uyw
 • Tarehe 19.10.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/12uyw