1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya Champions League yarejea

Bruce Amani
5 Machi 2018

Liverpool inajimwaga uwanjani ikipambana na FC Porto ya Ureno katika mpambano ya mkondo wa pili wa champions League

https://p.dw.com/p/2tjX1
UEFA Championsleague - FC Porto vs Liverpool
Picha: Reuters/M. Childs

Ushindi  wa  mabao 5-0 dhidi  ya  Porto  mwezi uliopita uliihakikishia Liverpool nafasi  katika  robo  fainali  lakini kocha  wa  Liverpool Juergen Klopp  amesema  atateua  kikosi imara kwa  mchezo  huo  licha  ya  kuelekea  Manchester United mwishoni mwa  juma.  Watapambana , ndicho  watakachokifanya. Ni  Wareno na  wanajihisi  fahari  na  watataka  kupambana. Wanataka  kulipiza kisasi. Amesema  Klopp  kuhusiana  na  mchezo  wa  kesho.  Lakini pambano  linalosubiriwa  kwa  hamu  hapo  kesho  ni  baina  ya Paris Saint Germain  na  Real Madrid. Baada  ya   ushindi  mnono wa  mabao 3-1  wa  Real Madrid  dhidi  ya  PSG  katika  mchezo  wa kwanza, mchezo  huo una  viashiria vyote  kwamba  moto  utawaka wakati  PSG ikitaka  kuonesha  kwamba  wanaweza  na  wako tayari  kulinyakua  kombe  hilo.

Real Madrid Toni Kroos Luka Modric
Real Madrid wana kibarua mjini Paris dhidi ya PSGPicha: picture-alliance/Zuma/J. Abuin

Lakini kikosi  cha  PSG kitamkosa kiungo nyota  mchezeshaji Neymar  ambaye aliondolewa  kutoka  hospitali  jana  Jumapili  kwa helikopta , siku  moja  baada  ya  kufanyiwa  upasuaji , na  kuanza hatua  za  kupona kabla  ya  kurejea  na  kujiunga  na  kikosi  cha Brazil  katika  kombe  la  dunia mwaka  huu.  Kijana  huyo  mwenye umri  wa  miaka  26 kiungo  mchezeshaji  wa  Paris Saint Germain alipelekwa katika  uwanja  wa  ndege  wa  Belo Horizonte kwa helikopta, ambako alikotarajiwa  kwenda  katika  nyumba  yake  ya kifahari  katika  mji  wa  kitalii  wa  Mangaratiba kiasi  ya  kilometa 100  kutoka  mjini  Rio de Janeiro.

Jumatano itakuwa  zamu  ya Tottenham Hot Spurs ikiikaribisha  Juventus Turin  na  Manchester City itakwaana  na Basel  ya  Uswisi.

Urusi inawanyamazisha  wenye  viwanda  vikubwa  ambao  wana hofu  na  kuonekana  kuvifunga  viwanda  kadhaa  vikubwa kuepusha  ajali na  kitisho cha  mashambulizi  ya  kigaidi  wakati  wa mashindano  ya  kombe  la  dunia  mwaka  huu. Kusitisha uzalishaji kunaelekea  ni  hatua  ambayo  Urusi  inataka  kuichukua  ikiwa  ni inayoonekana  kuwa  Urusi  iko  tayari  kupoteza  mapato  wakati itakapokuwa  mwenyeji  wa  mashindano  hayo  ya  kandanda  kwa mara  ya  kwanza  nchini  humo  kuanzia  Juni  14.

Mwandishi: Sekione  Kitojo /  dpae / rtre / afpe
Mhariri: Yusuf Saumu