1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya Bundesliga kupamba moto

12 Februari 2016

Ligi kuu ya kandanda Ujerumani - Bundesliga inaendelea wikendi hii ambapo Mabingwa watetezi Bayern Munich wangali bado kileleni katika orodha ya msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 53 kibindoni

https://p.dw.com/p/1HuZp
Deutschland Serdar Tasci Neuzugang FC Bayern München
Picha: picture-alliance/dpa/A. Gebert

Wakati Bayern watakuwa uwanjani Jumapili wakiwa wageni wa Ausburg, sawa na Borrusia Monchen gladbach itakayoumana na Hamburg , miongoni mwa michuano ya Jumamosi ni pamoja na ule kati ya Borussia Dortmund inayoshika nafasi ya pili pointi 8 nyuma ya Dortmund itakayopambana dhidi ya Hannover inayokamata mkia ikiwa nafasi ya 18, wakati Hertha Berlin ilioko nyuma ya Dortmund katika nafasi ya tatu kwa tafauti ya pointi 2 wakikaribishwa na Stuttgart . Michuano mengine ni Bayer Leverkusen dhidi ya Darmstadt .

FC Cologne leo ni wenyeji wa Eintracht Frankfurt, Wolfsburg pia wako nyumbani kuumana na Ingolstadt, huku Werder Bremen inayokabiliwa na hatari ya kushuka daraja, ikiumana na Hoffenheim , kilabu nyengine inayokabiliwa na janga hilo. Hoffenheim itaingia uwanjani leo ikiwa bila ya kocha wao Mholanzi Huub Stevens ambaye amejiuzulu m kwa sababu ya matatizo ya moyo ambapo itabidi afanyiwe upasuaji.

Stevens mwenye umri wa miaka 62, alikuwa na mkataba hadi mwishoni mwa msimu huu na alitangaza uamuzi wake katika mkutano na waandishi habari, akisema amegunduliwa kuwa na matatizo ya mapigo ya moyo. Amewahi pia kuwa mwalimu wa kilabu ya Schalke , Hertha Berlin ,Cologne, Hamburg, PSV Eindhoven ya Uholanzi na PAOK Thessaloniki ya Ugiriki.

Mwandishi: Mohamed AbdulRahman/AFP
Mhariri: Mohamed Khelef