Michezo | Matukio ya Kisiasa | DW | 05.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Michezo

Benin kama Nigeria na I.Coast kupata kocha mjerumani-Farbisch.

Baada ya simba wa nyika- Kameroun na Super Eagles, Nigeria,Benin itakua timu ya 3 itakayoteremka uwanjani na kocha wa kijerumani katika kombe la Afrika la mataifa mwezi ujao nchini Ghana.

Allan Wanga,ni mkenya wa kwanza kuajiriwa katika Ligi ya Angola. Anajiunga na mabingwa Petro Atletico. Nae Marco van Basten,hatakua tena kocha wa Holland baada ya kombe lijalo la Ulaya.Glasgow Celtic yawafuata mabingwa AC Milan katika duru ijayo ya champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya:

Kocha mjerumani Reinhard Fabish anatazamiwa kuteuliwa hivi punde kuwa kocha wa Benin kwa kombe la mwezi ujao la Afrika la mataifa nchini Ghana-hii ni kwa muujibu wa mkurugenzi wa shirikisho la dimba la benin alivyoarifu jana.

Fabish-kocha wa zamani wa Zimbabwe na Harambee Stars (Kenya) amependekezwa usoni yeye kuliko makocha 2 wa kifaransa kwavile shirikisho la kabumbu la Benin laamini furbish ana ujuzi zaidi.

Farbisch anakabiliwa na mtihani wa kuichukua benin hadi alao duru ya pili ya kombe la Afrika la mataifa kutoka kundi B linalojumuisha Nigeria,chini ya kocha mwengine wa kijerumani Berti Voigts na Tembo wa Corte d’Iviore chini ya kocha 3 wa Ujerumani Stielecke.

Kinyan’ganyiro hicho cha kombe la Afrika la mataifa kinaanza Januari 20 hadi finali Februari 10 mwaka 2008.Ghana na Guinea zitafungua dimba.

Jogoo la simba wa nyika-Kameroun, Samuel Eto’o limetangazwa sasa fit kurudi uwanjani baada ya kukaa nje ya chaki ya uwanja kwa miezi 3.Jumapili hii, Eto’o ataongoza hujuma za FC Barcelona dhidi ya Deportivo la coruna.Kurudi uwanjani kwa Eto’o, ni habari pia nzuri kwa mashabiki wa Kameroun.

Kenya, inayofunga dimba jumamosi hii na Taifa Stars ya Tanzania katika kinyan’ganyiro cha kombe la Cecafa la challenge cup huko Tanzania,staid wake wa kwamnza kucheza katika Ligi ya Angola na mabingwa Petro Atletico, ni Allan Wanga.Wanga amefungishwa mkataba akiwa mkenya wa kwanza katika Ligi ya Angola kwa kitita cha dala 15.000.Wanga ni chipukizi wa miaka 21.

Kocha wa Holland atakeiongoza katika kombe lijalo la ulaya la mataifa huko Uswisi na Austria mwaka ujao,Marco van Basten, ametangaza kuwa atan’gatuka mara tu kombe hilo likimalizika.Baada YA KIPINDI CHA MIAKA4,ITAKUA WAKATI UMEWADIA-ASEMA MSHAMBULIZI HUYO WA ZAMANI WA Holland kuchukua jukumu jengine.van Basten alichukua wadhifa huo kutoka kwea Dick Avocaat na kuiongoza Holland katika Euro 2004-kombe la ulaya 2004 nchini Ureno.

Viongozi wa Bundesliga-ligi ya Ujerumani Bayern Munich,wameamua kumuachia mlinzi wa taifa wa Ufaransa Valerien Ismail kujiunga na Hannover 96.Ismail, amekuwa nje ya chaki ya uwanja kitambo kirefu bila kuchezeshwa na B.Munich.

Nae mtaliana Felipo Inzaghi, aliibuka jana mtiaji magoli mengi kabisa katika dimba la ulaya akimvunjia rekodi hiyo mjerumani Gerd Mueller wa Bayern Munich.Bao lake jana dhidi ya Celtic ya Scotland, lilivunja rekodi hiyo na kuifungulia mlango tangu AC Milan hata Celtic kucheza duru ijayo.Ilikua pasi maridadi kutoka kwa Kaka na kutupiwa Cafu kabla Inzaghi kulifumania lango la Celtic kuweka rekodi hiyo mpya.

 • Tarehe 05.12.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CXXQ
 • Tarehe 05.12.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CXXQ

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com