Michael Schumacehr ashindwa kuwika Suzuki | Michezo | DW | 09.10.2006
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Michael Schumacehr ashindwa kuwika Suzuki

Wakati macho ya mashabiki wa Ujerumani yalikodolewa Suzuki,Japan kuona iwapo Schumacher angetamba na kutoroka na taji lake la 8 la mbio za magari,dimba lilitawala Ulaya na Afrika katika vinyan'ganyiro vya kuania tiketi za 2008 huko Uswisi na Ghana.

Nahodha wa Ujerumani Ballack baada ya 2:0 dhidi ya Georgia

Nahodha wa Ujerumani Ballack baada ya 2:0 dhidi ya Georgia

Katika Kombe la Ulaya la mataifa,mabingwa wa dunia Itali, wataokwa na jasho kabla kuitoa Ukraine;makamo-bingwa–Ufaransa wanaswa na mtego wa Scotland na Ujerumani yatamba mbele ya Georgia.

Katika mbio za magari,Michael Schumacher,azika ndoto ya ubingwa wa 8 wa dunia kabla kustaafu.Hayo na mengineo,ndio niliowaandalia jioni hii.

Tukianza na kinyan’ganyiro cha kuania tiketi za finali ya kombe la Ulaya 2008 nchini uswisi, kocha wa Ujerumani Joachim Loew aliwasaidia wajerumani mwishoni mwa wiki kusahau haraka kuondokewa na kocha Jürgen Klinsmann baada ya kombe la dunia.Ujerumani iliikomea Georgia mabao 2:0 na huo ni ushindi 4 mfululizo chini ya kocha mpya Loew.

Mabingwa wa dunia Itali pia chini ya kocha mpya Donadoni, ilitokwa na jasho kweli kabla hawakuizika Ukraine mjini Roma kwa mabao 2:0.Itali iliufumania kwanza mlango wa Ukraine mnamo dakika ya 71 ya mchezo kwa mkwaju wa penalty aliouchapa Massimo Oddo.

Luca Toni, aliechezewa ngware aliongeza bao la pili dakika 8 baadae.

Scotland iliwatia munda lakini makamo-bingwa wa dunia-Ufaransa baada ya kwatia scindo kubwa na mwisho kuwakomea bao 1:0.

Black Stars-Ghana ambayo ndio mwenyeji wa kombe lijalo la Afrika la mataifa 2008 ikiwa ziarani barani asia, iliikomea jan a Korea ya Kusini kwa mabao 3:1.Huo ulikuwa ushindi wapili wa Black Stars baada ya kuilaza Japan bao 1:0 jumatano iliopita mjini Yokohama.

Barani Afrika kwenyewe,timu kadhaa za taifa zilikuwa uwanjani kuania tiketi zao kwa finali za kombe la Afrika 2008:wasi wasi mkubwa ulikuwa kwa Afrika kusini,wenye wa kombe lijalo la dunia n a la kwanza afrika:Je, wangetamba Lusaka, dhidi ya wenyeji Zambia ?

Jawabu ndio, kocha wao mpya mbrazil Carlos Alberto akiwa pamoja nao kuwatia shime, Bafana bafana waliilaza Zambia kwa bao 1:0.Nahodha wao Aaron Mokoena, aliwapatia Afrika Kusini bao la kichwa kipindi cha kwanza cha mchezo na kumaliza udhia.Laiiti ingelishindwa,Afrika Kusini ingelijikuta pointi 5 nyuma ya Zambia.

Hatima ya Harambee Stars ilikatwa Luanda:Flavio alipiga hodi mara 2 katika lango la Kenya na kukaribishwa.Mwishoe, Kenya ilirudi Nairobi na mabao 3:1kikapuni mwake.Angola ilishinda mpambano wa kwanza dhidi ya Swaziland na inaongoza kundi hili kwa pointi 3.

Burundi na Ruanda ziliondoka tofauti katika mapambano yao kama vile Bakari Ubena anavyosimulia kutoka Bujumbura:

Jana ilikua zamu ya Cologne marathon hapa Ujerumani lakini ilikua mbio za kim 20 huko Hungary zilizokodolewa m acho zaidi.Nchini Hungary, mzaliwa wa Kenya anaekimbia chini ya bendera ya Holland, Kiplagat alishinda mbio za kwanza kabisa za km 20 za ubingwa wa dunia kwa muda wa rekodiya dunia.Kiplagat alichukua muda wa saa 1,dakika 3 na sek.21 kuvunja rekodi ya muingereza Paula Radcliffe.

Katika mbio za magari za Grand Prix huko Suzuki, mambo yalienda kombo kwa bingwa mara 7 wa dunia,mjerumani Michael Schumacher.Kwani, ushindi jana huko Japan ulienda kwa hasimu yake Fernando Alonso anaeongoza sasa kwa pointi 10 baada ya kuwa pointi 2 nyuma ya Schumacher.

Schumacher alibidi kuziacha mbio hizo katika hatua ya 37 baada ya kuharibikiwa na mshine ya gari lake la ferrari.Mwenzake Felipe Massa, lakini alikuja wapili na hivyo amebakisha matumaini kidogo kwa magari ya ferrari kunyakua taji la waundaji magari.Mbio za mwisho msimu huu zitakua Brazil na ndizo zitakazo mtawaza bingwa ditini-zaidi Alonso kuliko Schumacher inavyoonekana sasa.

 • Tarehe 09.10.2006
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHd4
 • Tarehe 09.10.2006
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHd4