Miaka kumi ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
15 Oktoba 2009Matangazo
Imetolewa tathmini mbali mbali
kuhusu taifa la Tanzania lilivyoelekea baada ya kifo cha mwanasiasa
huyo ambaye alitajikana hata nje ya mipaka yake, hasa katika siasa
zake za ujamaa na kujitegemea na kutaka viongozi wajiwekee miko
ukilinganisha na raia wengine. Othman Miraji alizungumza kwa simu
na Dr. Mohammed Bakari, mhadhiri mwandamizi katika chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, na kumuuliza kama kweli Tanzania ilivyo sasa ni
ile ambayo marehemu Nyerere alikuwa ana matumaini ya kuwa
nayo....