Miaka 4 leo tangu vita vya Irak | Magazetini | DW | 20.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Miaka 4 leo tangu vita vya Irak

Wahariri wa magazeti ya ujerumani walituwama leo hasa juu ya mada 2:Mpango wa marekani wa kutega makombora yake Ulaya ya mashariki na ukumbusho wa miaka 4 tangu vita vya Irak kuripuka:

Tukianza na miaka 4 leo tangu Marekani kuongoza majeshi ya muungano kuivamia Irak na kuutimua utawala wa Saddam Hussein, gazeti la STUTTGARTER ZEITUNG laandika:

“Vita dhidi ya Saddam viliandaliwa kwa hoja za uongo na zisizo na msingi.

Kipindi baada ya vita hakijazingatiwa kamwe na Washington wakati ule.Mtu alitarajia wairaki kama wajerumani baada ya vita vya pili vya dunia 1945,wangekaribisha mikonomiwili wakombozi wao.

George Bush alijihisi amejiweka safu moja na Rooservelt-mmoja kati ya marais maarufu wa marekani.Kwamba Bush si mtu apendae kufuata nasaha na mashaurti aopewayo na hawezi kuungama makosa na kurekebisha mkondo wa sera zake,hatojali maoni ya watu duniani na badala yake atajizatiti katika Ikulu (White House) akiufumbia macho ukweli wa hali ya mambo nchini Irak.”

Gazeti la HANDELSBLATT kutoka Dusseldorf laandika:

“Wamarekani wamegawika kuhusu msimamo gain wachukue .Kwanini, lauliza gazeti ? Kwa sababu, hakuna njia nyengine bora ya kujitoa katika janga hilo.Njia mbali mbali za kutoka Irak ni aina nyengine tu ya suluhisho lisiloridhisha.Ufa umepita kati kati ya kambi 2 kuu za kisiasa.

Bawa la shoto la chama cha Democrat laweza kudai kwa kasi kuohamishwa majeshi ya Marekani nchini Irak,kwavile chama hicho hakibidi kujitwika jukumu la hatua hiyo kwa kadiri kamanda mkuu wa majeshi anabakia kuwa George Bush.

Kuona Hilary Clinto,mtetezi mkuu wa Democrat kwa kiti cha urais hakubaliani na dai hilo la kun’gatuka Irak kutoka chama chake,anajipatia heshima.Lakini ,kuchukua msimamo unaoshikamana na ukweli wa mambo nchini Irak ni swali la uaminifu.”-

Ama gazeti la Frankfurter Rundschau linaona vita ilivyonadi marekani duniani kote dhidi ya chochote kile kilichotoa sura ya ugaidi,ndio madhambi makubwa iliofanya.Hii imewawezesha magaidi hasa na wanaowahurumia kuhisi wanahujumiwa bila ya sababu….”

Likituhetimishia mada hii, gazeti la BERLINER KURIER laandika kwamba George Bush alivitaka vita vya Irak na akafanya kila awezalo kuviendesha.Kwa kutapakaza uwongo na udanganyifu alipika jungu la vita hivyo na bila ya ridhaa ya UM.Kwa Marekani havikuwa mteremko,kwani badala ya kupokewa kwa maua ,wairaki sasa wanawaapiza wamarekani. Wanawaangalia ni watu walioikalia nchi yao na sio walioikomboa.Badala ya kufurahia demokrasi,wanabidi kujiwinda kuishi na vitisho.

Vita vya Irak vimegeuka kuwa jiinamizi la bahari ya damu.Bosh alijingiza Irak ili kuwatoa wairaki katika enzi za kale na kuwatia enzi mpya ya kisasa.Bush ataondoka na kuwarudisha wairaki katika enzi za kale kabisa.

Likitugeuzia mada gazeti la PFORZHEIMER ZEITUNG lazungumzia mpango wa Marekani wa kutega makombora ya kukinga roketi za adui Ulaya ya Mashariki.Laandika:

“Bibi Angela Merkel anahimiza kuwa mpango huo wa Marekani ujadiliwe ndani ya shirika la ulinzi la NATO.Lakini, Bibi Merkel anapaswa kudai zaidi akiwa kama mwenyekiti wa sasa wa UU.Anabidi pia kuuwajibisha UU barabara ndani ya mpango huo.Haifai kuona nchi zanachama wa UU kama Poland na Jamhuri ya Czech, zinajifanyia mambo pekee na kutojali masilahi ya ulinzi ya Umoja mzima wa Ulaya.

Isitoshe, haifai kusahau kuwa UU na hasa Bibi Angela Merkel ambae ana usuhuba mwema tangu kwa rais Putin hata kwa Bush aweza tena kuchangia kuleta mafahamiano bora kati ya Moscow na Washington.”