Mgomo wa reli nchini Ufaransa | Masuala ya Jamii | DW | 14.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Mgomo wa reli nchini Ufaransa

Usafiri umepooza leo kote nchini Ufaransa na hasa mjini Paris.Reli zimepunguza mno usafiri na abiria wanapata shida.Inatumainiwa mgomo huu hatahivyo, hautadumu muda mrefu.

Sarkozy akiwa Berlin-mgomo Paris

Sarkozy akiwa Berlin-mgomo Paris

Misafara ya reli nchini kote Ufaransa na usafiri wa abiria mjini Paris na vitongoji vyake, imeathiriwa mno hii leo na mgomo.Kumekuwapo ishara hatahivyo, kwamba tangu serikali hata vyama vya wafanyikazi wanasaka njia ya kuepusha mgomo mrefu.Mzizi wa fitina ni mabishano juu ya mageuzi ya mfumo wa bima ya malipo ya uzeeni.

Wafanyikazi wa shirika la RATAP linalotumikia usafiri wa jiji la Paris, walijiunga leo na mgomo huu ulioanzishwa jana jioni na wenzao wa shirika la wafanyikazi za reli SNCF.Waziri wa kazi wa Ufaranya Xavier Bertrand ameanza mkutano na viongozi wa vyama vya wafanyikazi hao kusaka suluhisho la mageuzi yaliopangwa na serikali juu ya mfumo wa malipo ya uzeeni .

“Nakisaka kituo changu chatreni,kwani hii asubuhi ya pirika-pirika nyingi na kuna treni 2 tu za kuweza kupanda.”

Yule ambae anaefungua leo radio au kuangalia TV husikia jambo moja tu:

“Ili kukusaidia,kuna simu maalumu za kupiga kujipatia taarifa.Ikiwa wataka kusafiri na Metro piga simu Namba: 0800151111.”

Kiongozi wa chama kikubwa cha wafanyikazi CGT,Bernard Thibault,jana alifungua njia ya mazungumzo aliposema yutayari kujadiliana na sekta maalumu zilizoathirika na mgomo wao wakati serikali nayo imeridhia dai lake kuwa nayo ishiriki katika majadiliano hayo.

Mageuzi hayo yanayopendekezwa na serikali ya rais Sakorzy, yanakomesha mtindo wa malipo maalumu ya uzeeni ulioanzishwa miaka ya 1930ini kwa wafanyikazi wa shirika la reli na nishati wa kjuwafidia kwa kazi zao ngumu.

Kiasi cha wafanyikazi 500,000 wanafaidika hivi sasa na mfumo huo.Kwa muujibu wa shirika la wafanyikazi za reli la SNCF ni 1 kati ya magari-moshi ya mwendo wa kasi 8 yanayokwenda wakati huu huku teeni zinazosafiri mikoani zikiathrika mno zaidi na mgomo.

Mjini Paris,ni 1 tu kati ya magari 5 ya chini y