Mgomo wa majaji nchini Uganda | Matukio ya Kisiasa | DW | 07.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mgomo wa majaji nchini Uganda

Mawakili kutoka Kenya na Tanzania wameungana na wenzao kuunga mkono mgomo wa majaji unaoendelea nchini humo.

Kizza Besigye wa chama cha upinzani Uganda

Kizza Besigye wa chama cha upinzani Uganda

Mawakili nchini humo wataanza mgomo wao wiki ijayo kuwaunga mkono majaji waliosusia kazi kupinga kile wanachodai uvamizi usio wa halali uliofanywa na vikosi vya usalama vya Uganda dhidi ya mahakama kuu na kukamatwa kwa watu sita wa chama cha upinzani nchini Uganda waliokuwa wameshtakiwa pamoja na kiongozi wa upinzani Kizza Besigye kwa madai ya kupanga njama za uasi dhidi ya serikali. Majaji walikutana leo kupanga mikakati wanayotaka serikali ichukue juu ya mustakabali wa usalama wa mahakama.

Saumu Mwasimba amezungumza na wakili Monica kutoka tume ya kimataifa ya wanasheria ambaye yuko Uganda kwa sasa kwa ajili ya mgomo huo na kumuuliza kwanini anaunga mkono mgomo huo.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com