1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa madereva wa treni nchini Ujerumani

12 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GW

Berlin:

Shughuli za usafiri wa treni zimevurugika nchini Ujerumani kufuatia mgomo wa madereva wa treni.Katika baadhi ya majimbo takriban nusu ya safari zote za treni zimesita.Wawakilishi wa shirika la wafanyakazi la GDL wanazungumzia juu ya kusitishwa shughuli nyingi za usafiri.Safari za treni zinazokwenda nje ya Ujerumani,hazikuathirika na mgomo huu.Wakati huo huo dalili zimeanza kuchomoza za kupatiwa ufumbuzi mvutano kati ya waajiri na waajiriwa.Pande hizo mbili zimekubaliana kurejea tena katika meza ya mazungumzo.Shirika la usafiri wa reli la Ujerumani linapanga kutoa pendekezo jipya la nyongeza ya mishahara jumatatu ijayo.