Mgomo wa Madaktari nchini Tanzania
12 Julai 2012Matangazo
Hali bado ni tete hasa baada ya Rais wa chama cha madaktari Dk. Namala Mkopi kufikishwa mahakamani kwa madai ya kuchochea mgomo, na serikali kufuta leseni za madaktari walioko katika mafunzo 390. Bruce Amani amezungumza na Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dr. Edwin Chitage ambaye kwanza ameelezea jinsi hali ilivyo.
(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Mohamed Abdulrahman