1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa kitaifa Ugiriki

6 Oktoba 2011

Polisi Ugiriki ilitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji mjini Athens, wakati wafanyakazi wa serikali na wanafunzi walipogoma dhidi ya hatua za kubana matumizi

https://p.dw.com/p/12mlT
Polisi ya kupambana na fujo kaziniPicha: dapd

Safari zote za ndege ziliahirishwa na treni zilisita kusafiri, wakati shule na mahakama zilifungwa.

Griechenland Streik Ausschreitungen Athen
Waandamanji wakipambana na polisi mjini AthensPicha: dapd

Serikali imetangaza kupunguza nafasi za ajira na mishahara, pamoja na kuongeza kodi, ili iweze kupata awamu nyengine ya mkopo wenye thamani ya euro bilioni 8.

Wakaguzi wa hesabu wa wakopeshaji wa kimataifa kwa Ugiriki, ambao ni Umoja wa Ulaya, Shirika la fedha la kimataifa, IMF, na benki kuu ya Ulaya, siku ya Jumanne waliahirisha uamuzi wa kutoa mkopo huo mwingine wakisisitiza kuwa Ugiriki itekeleza hatua zote zilizokubaliwa mwaka uliopita, ili iweze kupewa mkopo wa euro bilioni 110.

Griechenland Finanzkrise
Picha: dapd

Iwapo Ugiriki haitopokea mkopo huo wa euro bilioni 8 kufikia mwezi ujao, itashindwa kuwalipa wafanyakazi wa serikali na malipo ya pensheni.

Mwandishi Maryam Abdalla/alle