1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

 Mfumo wa uchaguzi Marekani

Zainab Aziz
8 Novemba 2016

Hata ingawa Marekani inafikiria kuwa ndio nchi inayo ongoza katika maswala ya Kidemokrasia, mfumo wake wa kumchagua rais si maarufu kwani hauwashirikishi raia moja kwa moja kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo  

https://p.dw.com/p/2SMHz
USA Wahlkampf um Präsidentschaft Kombi Anhänger Clinton / Trump
Picha: picture-alliance/AP Photo/R. D. Franklin/ G. Herbert

Kila jimbo nchini Marekani lina wajumbe kutegemea na idadi ya wapiga kura katika jimbo hilo. Kuna jumla ya wajumbe 538  katika majimbo yote, katika midadi hiyo kuna wawakilishi 435, Maseneta 100 na kuna wawakilishi watatu kutoka Wilaya ya Columbia.  Idadi ya wajumbe maalum katika kila jimbo ni sawa na idadi ya wabunge kutoka kwenye jimbo husika kwa mfano katika jimbo la California kuna wajumbe 55 kwa hiyo idadi hiyo ni sawa wabunge wake wanao wakilisha bungeni mjini Washington.

Mgombea urais atahitajika kupata angalau  kura 270 za wajumbe maalum ili kuweza kushinda kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani.  Hadi kufikia sasa chaguzi 57 za urais zimefanyika nchini Marekani ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa mwaka 2000 wakati ambapo wagombea walikuwa Al Gore wa chama cha Democratic dhidi ya George W Bush wa Republican ambapo Bush aliibuka kuwa rais wa Marekani hata ingawa Al Gore ndie aliyepata kura laki 5 na elfu 40 zaidi alizopigiwa na wananchi wa Marekani lakini kwa kuwa hakupata idadi kubwa ya kura za wajumbe maalum basi hakuweza kuchukua hatamu za uongozi kutokana na mfumo wa uchaguzi wa Marekani ambapo katiba inawapa nguvu wajumbe maalumu kuamua ni mgombea yupi atakae iongoza nchi hiyo.

USA Präsidentschaft Wahlkampf
Mfuasi wa mgombea mmoja wa uraisPicha: Reuters/M. Segar

Namna anavyochaguliwa rais ni kizunguzungu. 

Vile vile mwaka 1824 John Quincy Adams alishinda urais kwa kupigiwa kura nyingi na wajumbe maalum hata ingawa mpinzani wake  Andrew Jackson alimshinda kwa kura elfu 40 zaidi kutoka kwa wananchi.  mwaka 1876  Samuel Tiden alishinda kwa wingi wa kura zaidi ya laki 2 na nusu dhidi ya mpinzani wake Rutherford Hayes lakini kamati maalum iliamua kumpa ushindi Hayes kulingana na misingi ya kichama na ambapo baadaye liliundwa jopo kuchunguza makosa ya uchaguzi.

Mwaka 1888 Grover Cleverland alimshinda mpinzani wake Benjamin Harrison kwa kura zaidi ya elfu 90 alizopigiwa na wananchi lakini wajumbe maalum walimpa uongozi Harrison.

Wakosoaji wa maswala ya kisiasa wanaukosoa mfumo huo wa kuchaguliwa rais wa Marekani na wajumbe maalum, wanasema umepitwa na wakati na kwamba unastahili kubadilishwa kwa kufwata matokeo halisi ya kura zilizopigwa na wananchi.  wanautaja kuwa kuwa unafedhehi mfumo mzima wa upigaji kura na hasa kwa wapiga kura wenyewe. Wajumbe maalum wanapinga vikali tuhuma hizo.

Mwandishi: Zainab Aziz/DPAE

Mhariri: Gakuba Daniel