1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme wa Ubeligiji atatua mzozo wa kisiasa katika miliki yake

21 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CehO

BRUSSELS:

Mfalme wa Ubeligiji amemteua waziri mkuu wa zamani –Guy VERHOFSTADT aendelee na serikali ya mpito yenye lengo la kuiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.Serikali ya mpito inaapishwa hii leo. Serikali ya muungano wa vyama vitano, inamaliza mvutano wa kisiasa ambao umeendelea kwa mda wa siku 195. Mgogoro huo umezusha tetesi kuwa huenda Ubelgiji ikagawanyika baina ya majimbo yanayozungumza kifaransa na Kiflemish.