1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MEZT: Watu 12 wauwawa katika ajali ya treni

11 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3n

Watu takriban 12 wameuwawa leo na wengine 21 wamejeruhiwa katika ajali ya treni karibu na kijiji cha Zoufftgen kaskazini mwa Ufaransa. Ajali hiyo ilitokea wakati treni ya abiria ilipogongana na treni ya mizigo katika eneo hilo.

Duru zinasema abiria tisa, wafanyakazi wawili wa treni na mtu mmoja aliyekuwa akiyafanyakazi ya reli ni miongoni mwa waliouwawa. Ajali hiyo imetokea karibu na mpaka kati ya Ufaransa na Luxembourg.

Treni ya abiria ilikuwa njiani kuelekea mjini Nancy Ufaransa ikitokea Luxembourg, ilipogongana na treni ya mizigo iliyotokea mjini Thionville Ufaransa ikielekea Luxembourg.

Ajali hiyo imetokea mahala ambapo ukarabati wa reli ulikuwa ukiendelea.

Inahofiwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka huku baadhi ya abria wakiwa bado wamekwama ndani ya mabehewa.