Wakati Mexico ikikosoa hatua ya Rais Donald Trump kupeleka wanajeshi mpakani, wachambuzi wanasema huenda pia bunge la Marekani likakataa kuidhinisha amri yake ya kuvipeleka vikosi vya ulinzi mpakani. Sylvia Mwehozi amezungumza na Profesa Patrick Nigula aliyeko chuo kikuu cha South Carolina Marekani, kwanza alimuuliza uamuzi huo utamaanisha nini kwa nchi hizo mbili.