1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MEXICO: Kimbunga Paul chakaribia kupiga nchini Mexico

24 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCze

Wakaazi wa eneo la rasi ya Baja California nchini Mexico, wanajiandaa kukabiliana na kimbunga kwa jina Paul, ambacho kinakaribia eneo hilo. Kimbuga hicho kinasonga mbele kwa kasi ya kilomita 135 kwa saa. Na wataalamu wa hali ya hewa wanasema huenda kimbunga hicho kikapita katika eneo la Baja California na kuzipiga sehemu za pwani za Mazatlan kabla ya kufikia kesho.

Eneo la Baja California limeshakumbwa na vimbunga viwili msimu huu.