1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mexico City. Calderon aapishwa kinyemela kuwa rais.

1 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnd

Felipe Calderon amechukua wadhifa wa urais , akiwa rais mpya wa Mexico katika sherehe ya ghafla iliyofanyika mapema leo. Hatua hiyo ilikuwa na lengo la kuzuwia upinzani katika baraza la Congress kutoka upande wa wabunge wa mrengo wa shoto ambao wanasisitiza kuwa ameshinda uchaguzi huo kwa wizi wa kura.

Hali ya wasi wasi imeongezeka nchini Mexico tangu pale mgombea wa kiti cha urais kutoka mrengo wa shoto Andres Manuel Lopez Obrador kushindwa uchaguzi wa Julai 2 kwa chini ya asilimia 1 ya kura.

Wabunge wa mrengo wa shoto wameapa kumzuwia kwa nguvu Calderon leo Ijumaa kukamilisha hatua ya kumuapisha katika baraza la Congress. Badala yake Calderon alichukua madaraka ya urais katika tukio ambalo halikutarajiwa , lililotangazwa moja kwa moja katika televisheni usiku wa manane siku ya Alhamis.