1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel aonyesha matumaini kuhusu Ugiriki

19 Juni 2011

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ameonyesha matumaini kuhusu mzozo wa madeni wa Ugiriki. Merkel ameliambia gazeti la Super Illu kuwa Ulaya ilikuwa imejiandaa zaidi kwa ajili ya siku zijazo kuliko miaka iliyopita.

https://p.dw.com/p/11eym
Kansela wa Ujerumani, Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa

Pia amepongeza maendeleo ambayo Ugiriki imeyafikia mwaka mmoja uliopita kuelekea kukabiliana na mzozo wake wa madeni, lakini amesema bado haijatosha.

Ujerumani na Ufaransa zimeahidi kuendeleza msaada wao wa kifedha kwa Ugiriki, lakini Ujerumani inataka wawekezaji binafsi wachangie katika mpango wa pili wa kuiokoa Ugiriki na madeni, ambao utajadiliwa baadae mwezi huu.

Euro-Gruppen-Präsident Jean-Claude Juncker warnt vor Übergreifen der Euro-Krise
Kiongozi wa mataifa yanayotumia sarafu ya Euro, Jean-Claude JunckerPicha: picture-alliance/dpa

Mwenyekiti wa kundi la mataifa yanayotumia sarafu ya Euro, Jean-Claude Juncker ameionya Ujerumani kutoyashinikiza mabenki binafsi yanayoshikilia hisa katika benki za Ugiriki kuchangia zaidi katika msaada huo.

Amesema hatua hiyo itasababisha mashirika ya uorodheshaji kuitangaza Ugiriki kuwa katika hali ya kutoweza kulipa madeni yake na athari zikiwepo kwa Ubelgiji na Italia.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (RTRE,DPAE,AFPE)
Mhariri: Maryam Abdalla