1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel akataa pendekezo la Sarkozy

6 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CY8D

BERLIN

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amelikataa pendekezo la Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa alilotowa nchini Algeria la kuwepo kwa umoja wa nchi za Mediterranean.

Merkel amesema ana hofu mpango huo unaweza kutishia Umoja wa Ulaya.Sarkozy mara ya kwanza aliwasilisha mpango wa kuwepo kwa umoja huo hapo mwezi wa Mei wakati alipopendekeza kwamba nchi zote zenye kupakana na bahari ya Mediterranean ziwe na mkutano wa viongozi chini ya urais wa kupokezana.

Merkel na Sarkozy wanatazamiwa kukutana mjini Paris leo hii kwa mazungumzo yasio rasmi.