Mbunge Ibrahim Abirige aliuwawa na watu wasiojulikana waliomfyatulia risasi akiwa ndani ya gari lake nyumbani kwake nje ya mji mkuu wa Kampala. Ni mmoja wa watu mashuhuri walioko katika orodha ya waliouwawa karibuni na watu wasiojulikana. Bunge linataka uchunguzi ufanyike haraka.