Je umewahi kufikiri kuwa baadhi ya takataka za nyumbani zinaweza kugeuzwa kutengeneza nguo za kuvaa katika tamasha za urembo? Ikiwa hukujua basi kutana na mwanamitindo kutoka Cameroon Ngwane Liz ambaye anatengeneza mavazi ya urembo kutumia takataka mbalimbali. Mradi ambao umefaulu nchini mwake.