1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya Super Tuesday yachunguzwa

7 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D3g1

WASHINGTON:

Nchini Marekani,wagombea nafasi ya kuwania urais wanachunguza matokeo ya kura zilizopigwa siku ya Jumanne katika baadhi kubwa ya majimbo nchini humo na sasa wanajitayarisha kwa duru nyingine mwishoni mwa juma hili.Upande wa chama cha Republican,Seneta John McCain amechomoza mbele ya wapinzani wake na ameahidi kukiunganisha chama hicho chini ya misingi ya kihafidhina na hivyo kuimarisha nafasi ya kuchaguliwa kugombea urais kwa tikti ya chama cha Republican.

Lakini katika chama cha Demokratik hakuna mshindi dhahiri aliechomoza.Hillary Clinton ameshinda zaidi katika majimbo yenye wakazi wengi kwa hivyo anaongoza kwa idadi ya wajumbe kulinganishwa na Seneta Barack Obama.Makundi yanayoshughulikia kampeni za Obama na Clinton yamekiri kuwa wagombea hao wawili wakiwa bega kwa bega,mchuano huo utakuwa mkali.