Matarajio ya mwaka mpya wa 2012 barani Ulaya | Magazetini | DW | 02.01.2012
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Matarajio ya mwaka mpya wa 2012 barani Ulaya

Matumaini kwa mwaka 2012,mbinu za Iran ,miaka 10 tangu sarafu ya pamoja ya Euro ilipoanzishwa na hali nchini Iraq ni miongoni mwa mada zilichambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

--- DW-Grafik: Per Sander/Peter Steinmetz

Wimbi la mageuzi katika nchi za kiarabu

Likimulika yaliyopita na kutathmini yanayoukabili mwaka mpya wa 2012,gazeti la "Süddeutsche Zeitung" laq mjini Munich linaandika:Mwaka 2011 ulikuwa mwaka wa mapinduzi,mwaka wa ghadhabu za wananchi na vuguvugu la wapenda mageuzi waliokuwa wakipaza sauti kudai maadili ya magharibi:Demokrasia,uwazi, na kuwajibika.Mwaka 2012 utadhihirisha hatima ya maadili hayo.Kwasababu mwaka huu wa 2012 utaleta changamoto kwa demokrasia.Wakati huo huo ni mwaka muhimu kwa mfumo wa mashindano unaozidi kudhibitiwa na China na Marekani.Ni mashindano kati ya  mfumo wa kidemokrasi na mfumo wa kiimla,vuguvugu la walio wengi dhidi ya uamuzi wa kutoka juu na uazi dhidi ya hadaa.

Titel: Ali Saiedie Beschreibung: Ali Saiedie Ali Saidi (Saidie), Stellvertreter des religiösen Führers Irans in der Revolutionsgarde äußert sich am Sonntag, den 1.1.2012 über den Hausarrest der beiden iranischen Oppositionsführer Mir Hossein Mousavi und Mehdi Karoubi. Lizenz: Mehr Geliefert von: Pedram Habibi

Mamullah wa Iran

Gazeti la Braunschweiger Zeitung linazungumzia juu ya mchezo hatari wa Iran na kuandika:Mbinu za kuvuta wakati zimeifikisha mbali Teheran,pengine mamullah hawaamini kama jumuia ya kimataifa inaweza kupitisha hatua zozote dhidi ya nchi yao.Wanacheza na moto.Hata kama Marekani inayoongozwa na Obama imechoshwa na vita,hata kama ulaya imezongwa na hofu za kiuchumi,watu hawastahiki kupuuza,si vitisho vya kinuklea dhidi ya Israel na nusu ya bara la Ulaya na wala si kile cha kuufunga ujia wa maji zinakopitia meli za mafuta katika ghuba la Uajemi.Vita vinaonyesha haviwezi tena kuepukwa.

Irak pia imegonga vichwa vya habari vya magazeti katika toleo la kwanza la mwaka mpya hii leo.Gazeti la "Märkische Allgemeine" linaandika:Maliki ndie kiongozi anaefaa kuiongoza Iraq,alisema George W. Bush mnamo mwaka 2006,aliporidhia Nouri al Maliki awe waziri mkuu .Chaguzi hazikusaidia kuleta wingi wa kura kwa upande wowote ,na Maliki alikuwa mgomboa wa maridhiano.Bush aliamini angeweza kutuliza mvutano kati ya waumini wa madhehebu ya sunni na wale wa madhehebu ya shiiya.Amekosea.Miaka yote miwili ya mwanzo ya kuwepo kwake madarakani imeshuhudia damu nyingi kabisa kumwagika kuliko wakati wowote ule mwengine wa historia ya hivi karibuni ya Iraq na mpango wa usalama wa Baghdad ulioandaliwa na jenerali wa kimarekani Petraeus umefanikiwa chupu chupu kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe visiripuke.Kwamba hivi sasa baada ya vikosi vya Marekani kuihama nchi hiyo,Nouri al Maliki anaendeleza bila ya wasiwasi mbinu zake za kuwatimua katika uwanja wa kisiasa,wasuni,si jambo la kustaajabisha.

Zerfallender Euro und EU-Fahne, Schuldenkrise in Europa

Umoja wa sarafu barani Ulaya

Mada yetu ya mwisho magazetini inamulika miaka kumi tangu sarafu ya pamoja ya Ulaya-Euro ilipoanza kutumika.Gazeti la "Lausitzer Rundschau" linaandika:Umoja wa sarafu umesalia jina linalosifiwa na wanasiasa bila ya kuwa na nguvu zozote za kisiasa kuweza kukiuka hisia za kitaifa.Anaetaka kuendeleza sarafu ya pamoja anabidi akubali sehemu kubwa ya madaraka yakabidhiwe halmashauri kuu ya mjini Brussels.La sivyo kanda ya Euro itavunjika.Sarafu ya pamoja inajikuta katika njia panda.

Mwandishi:Hamidou mOummilkheir/Inlandspresse

MhaririYusuf Saumu

 • Tarehe 02.01.2012
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Maneno muhimu Magazetini
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13coK
 • Tarehe 02.01.2012
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Maneno muhimu Magazetini
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13coK