1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashindano ya mbio za masafa mafupi Bahamas

11 Aprili 2015

Itakuwa ni zaidi ya zawadi za fedha na medali zitakazoshindaniwa katika mbili kati ya mbio za masafa mafupi maarufu zaidi katika Mashindano ya Ulimwengu ya Mbio za masafa mafupi za IAAF nchini Bahamas mwezi ujao

https://p.dw.com/p/1F6NH
Leichtathletik WM in Moskau 2013 Usain Bolt
Picha: Reuters

Washindi wanane wakuu katika mbio za wanaume na wanawake za mita mia moja wanariadha wanne kupokezana vijiti na mita mia nne wachezeji wanne kupokezana vijiti kwenye mashindano hayo ya mjini Nassau Mei 2 hadi 3 watafuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 2016. Hayo ni kwa mujibu wa Shirikisho la Riadha Ulimwenguni – IAAF.

Mwanariadha wa kasi zaidi ulimwenguni Usain Bolt atashiriki katika mashindano hayo mwaka huu. Nafasi nyingine nane zitachaguliwa kwa kutumia muda utakaowekwa na wanariadha. Mashindano hayo yanatarajiwa kuwashirikisha zaidi ya wanariadha 600 wanawake na wanaume katika vitengo vya 4x100m, 4x200m, 4x400m, 4x800m.

Wakati huo huo, Chama cha Riadha nchini Kenya kimetabgaza orodha ya mwisho ya timu itakayoiwakilisha Kenya katika mashindano hayo ya Bahamas.

Wanariadha 27 wa timu hiyo wanatarajiwa kuripoti katika kambi ya mazoezi wiki ijayo mjini Nairobi. Asbel Kiprop ni mmoja wa majina maarufu yaliyotajwa katika kikosi hicho, pamoja na Abednego Chesebe, Joseph Poghiso, Fergusson Rotich na Ronald Kwemoi. Kutokana na kukosekana kwa David Rudisha, Timothy Kitum ataongoza kikosi cha Alfred Kipketer, Nicholas Kiplagat, Jeremiah Mutai na Bernard Kipyegon.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Mohamed Dahman