1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashindano ya 12 ya riadha Berlin yamalizika.

24 Agosti 2009

Kenya imeibuka 3 na taifa kuu la riadha Afrka.

https://p.dw.com/p/JHRk
Kenenisa Bekele awika tena.Picha: AP

Mashindano ya 12 ya riadha ulimwenguni yalimalizika jana kwa kishindo kama yalivyoanza pale Kenenisa Bekele wa Ethiopia akitoroka na taji lake la pili katika mita 5000.

-Baada ya ushindi wa medalii ya dhahabu wa Caster Semenya ,Mulaudz ameipatiia Afrika kusini medalii yake ya pl ya dhahabu katika mbo za mita 800 wanaume.

-Bingwa wa duna wa mbiio hizo Alfred Yego ameipatia Kenya medalii ya fedha .

-Na jogoo la mashindano haya Usain Bolt wa Jamaica, asema kwamba, amefurahishwa mno na mashindano ya IAAF Berliin.

-Kenenisa Bekele wa Ethiopia,kama Usain Bolt wa Jamaica, wamepiga mhuri wao na kuandiika ukurasa maalumu katika kitabu cha mashindano haya ya ubingwa wa dunia.Bekele baada ya ushuindi wake wa mta 10.000,jana alitoroka na medali ya dhahabu katka mta 5000 ingawa altolewa jasho mno na mzaliwa wa kenya ,anaekimbiia chin ya bendera ya Marekanii,bingwa mtetez Bernard Lagat.Bekele alishinda pia mbio hizo mbili katiika mchezo ya Olimpik mwaka jana.

Jariibio la mzaliwa wa Kenya mwengine anaekimba chiini ya bendera ya Bahrein Yusuf Saad Kamel kutwaa taji la miita 800 baada ya liile la mita 1500 lilishindwa mfundoni.Aliondokea na medali ya shaba,ile ya dhahabu ikinyakuliwa na muafrka Kusini Mbulaeni Mulaudzi. Medal ya fedha katika changamoto hiyo ya mita 800 ilikwenda kwa aliekuwa bingwa wa mbiio hizo mkenya ,Alfred Yego.

Maryam Yusuf Jamal aliekimbia pia chini ya bendera ya Bahrein, alimaliza wapli katika mbio za mita 1500 wanawake, ambazo awalii ushindi alipewa mhspania Natalia Rodrguez.Kwavile, Rodriguez almtia munda muethiopa Gelete Burka, alekua akiongoza mbio hizo na kumuangusha, alivuliwa taji na kutawazwa Maryam Yusuf Jamal bingwa.

Nyota wa mashindano haya ya 12 mjni Berlin, bila shaka, alikuwa si mwengine, bali mjamaica Usain Bolt.Usain Bolt amenyakua medali 3 za dhahabu kutoka mashindano haya na ameweka rekodi 2 za duna na za ajabu katika mita 100 ya sek.9.58 na mita 200 kwa sek.19.19.Na mbali na zawadi ya sehemu ya ukuta wa Berlin altunukiwa na diwanii wa jiji hilo, Usain Bolt ,anaondoka Berlin kwa furaha kuu.

"Mambo yamekwenda uzuri kabisa.Nimevunja tena rekodi 2 za duna-nimefurahii sana."Usain Bolt.

Tugeukie sasa dimba na kabla hatujaikagua Lgi ya Tanzania ilioanza jana,

Katika Bundeslga-ligi ya Ujerumani, Bayer Leverkusen, iliparamiia kileleni mwa Ligi baada ya kuikomea Freiburg, Jumamosi mabao 5-0.Hamburg iliwapa mabingwa

Wolfsburg pigo lao la kwanza nyumbani tangu kupita mechi 20 walipowachapa mabao 4-2. Bayern Munich, mabingwa mara kadhaa wameeleza tena walipozabwa mabao 2-1 na chipukizi Mainz.Sasa Munich ina pointi 2 tu kutoka mechi 3. Kiti cha kocha wao mpya,mdachi Van Gaal kimeanza kutikisika.

Katika Premer League, Ligi ya Uingereza, Tottenham Hotspur wakitamba kwa mara ya kwanza mwanzo wa msimu tangu kutwaa vkombe vyote 2 ,1961, imeparamiia kileleni mwa ligi ya Uingereza kwa tofauti ya magoli kati yake na Chelsea.Hii iilifuatia ushindi wao jana wa mabao 2-1 huko Upton Park.Chelsea iilishinda 2-0 kwa jran zao Fulham kutokana na mabao ya Drogba na Anelka.

Katika Serie A-ligi ya Ital, Inter Milan iilanza kutetea ubingwa wake bila kutamba na kumudu sare ya bao 1-1 dhidii ya Bar.Mkamerun Samuel Eto-o ndie alewapatia bao lao.AC Milan lakini ilitamba kwa mabao 2-1 dhdi ya Siena.Ronaldinho alipendeza kwa kugawa pasi maridadi.

Muandishi: Ramadhan Ali

Uhariri: M-Abdulrahman