1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashabiki: Dortmund walikosa fursa kwa usajili wa Nmecha

Iddi Ssessanga
4 Julai 2023

Mashabiki wa Borussia Dortmund bado wana wasiwasi mkubwa kuhusiana na kusainiwa kwa mchezaji kiungo wa Ujerumani Felix Nmecha, licha ya rais wa klabu hiyo kusema anamuamini mchezaji huyo na uhamisho umekamilika

https://p.dw.com/p/4TOW7
Fußball Nationalmannschaft Deutschland - Frankreich
Picha: Jürgen Fromme/firo Sportphoto/picture alliance

Jarida maarufu la mashabiki wa Dortmund schwatzgelb.de lilichapisha makala siku ya Jumanne ikielezea kusikitishwa na uhamisho huo na kusema klabu hiyo ilikosa nafasi ya kuchukua msimamo wa wazi.

"Klabu ilikosa nafasi ya kuweka wazi kwamba hakuna kigezo cha michezo kingeweza kufidia mtu binafsi kukosa maadili muhimu zaidi ya klabu! Kauli hiyo muhimu ingewezekana, bila kujali uvumi huo," makala hiyo ilisoma.

Soma pia: Bayern wazivunja tena nyoyo za mashabiki wa Dortmund

Kuwasili kwa Felix Nmecha kulikuja katikati mwa ukosoaji kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa Dortmund, baada ya mchezaji huyo kutoa machapisho ya mitandao ya kijamii ambayo yalichukuwa kuwa ya chuki dhidi ya mashoga, yakielekezwa dhidi ya jumuiya ya LGBTQI+, na isiyoendana na maadili ya Dortmund.

Dortmund vor dem Meisterschaftsfinale
Mashabiki wa BVB bado wasiwasi kuhusu usajili wa Nmecha.Picha: Federico Gambarini/dpa/picture alliance

Iligharimu vizazi kabla yetu nguvu nyingi na juhudi na wakati "kuhakikisha kwamba kila mmoja" anaweza kujiskia anakaribishwa katika familia ya Dortmund," aliandika mwandishi, na kuongeza kuwa hata "hajui ikiwa kutojua ndiyo neno sahihi kwa kile ambacho klabu imefanya."

Rais wa Dortmund Reinhold Lunow alituma ujumbe kwenye Twitter mwishoni mwa Jumatatu kwamba "mimi pia, hapo awali nilikuwa na mashaka makubwa kuhusu kama anashiriki maadili ya Borussia yetu. Kwa sababu hii, ilikuwa muhimu kwangu kumfahamu yeye binafsi."

Soma pia:Dortmund yaizaba Augsburg na kukamata usukani wa ligi 

Lunov na mkurugenzi mtendaji wa Dortmund Hans-Joachim Watzke walikuwa na mkutano na mchezaji huyo ili kuzungumza juu ya imani na maadili yake kabla ya mkataba huo kukamilika Jumatatu wakati Nmecha alipotia saini mkataba wa miaka mitano na washindi hao wa pili wa Ligi ya Bundesliga akitokea Wolfsburg, katika hatua inayotajwa kuwa na thamani ya takribani euro milioni 30, sawa na dola milioni 32.7.

"Katika mazungumzo ya moja kwa moja niliyofanya naye pamoja na Aki Watzke, alinihakikishia kwa hakika kwamba anashiriki maadili ya kanuni zetu za msingi na atafanya ipasavyo. Felix Nmecha atalazimika kuaminiwa na wachezaji wengi wa BVB kutokana na kukosolewa katika maandalizi ya uhamisho. Ana imani yangu."

Frankfurt | Vorstellung Rudi Völler als neuer Sportdirektor der A-Nationalmannschaft
Mtendaji Mkuu wa BVB, Hans-Joachim Watzke.Picha: Christopher Neundorf/Kirchner-Me/picture alliance

Nmecha aliyeichezea timu ya taifa ya Ujerumani Die Mannschaft mara moja alikuwa amesema hivi karibuni kwenye Instagram kwamba "Ninawapenda watu WOTE kwa dhati na sibagui mtu yeyote." Katika taarifa ya klabu Jumatatu, alisema: "Natumai mashabiki watanipa nafasi ya kunifahamu."

Kocha Edin Terzic alisema Dortmund wanataka kumuunga mkono Nmecha "katika kujiendeleza kama mchezaji wa soka na kama mtu. Tuna uhakika kwamba Felix anaweza kuwa sehemu muhimu ya timu yetu haraka sana."

Chanzo: DPAE