1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatangaza vikwazo kwa watu na makampuni chini Urusi

Lilian Mtono
14 Septemba 2023

Marekani imewekea vikwazo kwa watu 150 pamoja na makampuni kutoka Urusi hadi Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu, ikijaribu kudhibiti hatua za Kremlin kupata teknolojia, fedha kuendeleza vita vyake nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4WLUT
Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Hivi ni vikwazo vikubwa zaidi kutangazwa na Marekani na idara za wizara ya fedha, na vya karibuni zaidi kuwalenga watu na makampuni ya mataifa mbalimbali na hasa Uturuki ambayo ni mwanachama mwenzake wa NATO ambayo huiuzia Urusi tekenolojia ya magharibi  inayoweza kuchochea vita nchini Ukraine.

Soma pia:Marekani yaanza tena operesheni za kupambana na ugaidi Niger

Mkuu wa ofisi inayohusika na shughuli za uratibu wa vikwazo katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani, James O'Brien ameliambia shirika la habari la AP kwamba vikwazo hivyo vinalenga kuzuia uendelezwaji wa sekta ya nishati nchini Urusi pamoja na vyanzo vya kifedha katika siku za usoni kama miradi ya gesi asilia ya Arctic, uchimbaji madini na uzalishaji na ukarabati wa silaha za Urusi.