1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaishauri Nigeria kuwa na sarafu imara

Grace Kabogo
19 Septemba 2023

Naibu Waziri wa Fedha wa Marekani, Wally Adeyemo, ambaye anaizuru Nigeria kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na nchi za Afrika, ameishauri Abuja kuhakikisha inakuwa na sarafu imara na inapambana na ufisadi.

https://p.dw.com/p/4WX5n
USA Wilmington 2020 | Adewale Wally Adeyemo, nominierter Deputy Secretary of the Treasury
Picha: Alex Wong/Getty Images

Ziara yake mjini Lagos, inafanyika wakati ambapo Rais Bola Tinubu wa Nigeria anafanya mageuzi ya kuufufua uchumi wa nchi hiyo.

Naibu huyo wa waziri wa fedha wa Marekani alisema Nigeria inaweza kuwavutia moja kwa moja wawekezaji wa kigeni, ikiwa ingeliongeza juhudi za kuwa na sarafu imara, na kurekebisha sera zake za kifedha.

Soma zaidi: Upinzani utakata rufaa kupinga urais wa Tinubu Nigeria

Adeyemo aliishauri serikali ya Abuja kutumia rasilimali kutoka kwenye ruzuku ya mafuta ili kuwekeza zaidi katika miundombinu ya kidijitali, elimu, kilimo na mazingira imara ya biashara ndogondogo.

Ziara ya Adeyamo inafanyika, baada ya maafisa wengine wa ngazi ya juu wa Marekani kulitembelea bara la Afrika, akiwemo waziri wake wa fedha, Janet Yellen, na Makamu wa Rais Kamala Harris.