Marekani yahimiza uchaguzi uitishwe haraka nzuwani | Matukio ya Kisiasa | DW | 10.01.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Marekani yahimiza uchaguzi uitishwe haraka nzuwani

Marekanmi yaunga mkono juhudi za kuitishwa uchaguzi haraka katika kisiwa kinachoasi cha Komoro-Nzuwani

default

Fukwe za visiwa vya Komoro


Mod:


Marekani inaunga mkono duru mpya ya uchaguzi iitishwe haraka katika kisiwa kinachoasi cha Komoro-Nzuwani-hayo ni kwa mujibu wa mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Afrika.Zaidi anasimulia Oummilkheir.


"Tunaunga mkono moja kwa moja Umoja wa Comoro na Umoja wa Afrika katika juhudi zao za kuhimiza uchaguzi huru na wa haki uitishwe haraka iwezekanavyo kisiwani Nzuwani" amesema hayo waziri mdogo wa mambo ya nchi za nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Afrika bibi Jendayi Frazer,wakati wa mkutano pamoja na waandishi habari.


Alikua akizungumza mjini Moroni,katika ziara fupi katika visiwa hivyo vya bahari ya Hindi.


October 10 iliyopita,Umoja wa Afrika umeweka vikwazo vya usafiri na kuzuwia mali ya rais wa kisiwa cha Nzuwani Mohammed Bacar pamoja na maafisa wengine wa ngazi ya juu wa serikali yake ambayo serikali ya shirikisho la visiwa vya Komoro na Umoja wa Afrika unaitaja kua si halali.


Serikali kuu ya visiwa vya Komoro mjini Moroni imetishia kutumia nguvu ili kurejesha nidhamu kisiwani Nzuwani.


Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani bibi Jendayi Frazer amezungumzia pia masuala ya ushirikiano katika sekta ya usalama kati ya Marekani na Komoro.


"Hivi karibuni tumeiingiza Komoro katika mpango wa Mkakati wa kimkoa kwa eneo la Afrika Mashariki-mpango uliolengwa kuimarisha uwezo wa washirika wetu katika kupambana na ugaidi."Amesema bibi Frazer.


"Mpango huo unajumuisha mafunzo ya usalama wa mpakani na mwambao-utaratibu unaoimarisha shughuli za kukaguliwa watu na bidhaa katika maeneo ya mpakani na baharini."Amefafanua bibi Frazer.


Tulizungumza hivi punde na afisa wa ngazi ya juu wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Komoro anaeshughulikia masuala ya nchi za kiarabu bwana IBrahim Abdallah.kutaka kujua uhusiano ukoje kati ya serikali ya Marekani na Komoro,na alikua na haya ya kusema:


O-Ton.............


Marekani inamsaka raia mmoja wa Komoro Mohammed Abdullah Fazul anaetuhumiwa kuhusika na mashambulio ya mwaka 1998 dhidi ya ofisi za ubalozi wa Marekani mijini Daresalam na Nairobi.►◄

 • Tarehe 10.01.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CnRI
 • Tarehe 10.01.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CnRI

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com