Marekani kutumia dola bilioni 819 kuupiga jeki uchumi
29 Januari 2009Matangazo
Uamuzi huo umeungwa mkono kwa kura 244 za upande wa Demokratik na kupingwa na upande wa Republikan kwa kura 188.Rais Barack Obama wa Marekani alisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua hiyo ili kuyanusuru maisha ya raia wa kawaida
Mswada huo ulipingwa na wanachama 11 pekee wa Demokratik na kuungwa mkono na waliosalia.Upande wote wa Republikan uliupinga mswada huo.Mswada huo unasubiri kujadiliwa na Baraza la Senate wiki ijayo.