1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marais wa ECOWAS wawasili Abidjan

Aboubakary Jumaa Liongo28 Desemba 2010

Kiongozi wa Cote d´Voire Laurent Gbagbo anakabiliwa na changamoto mpya wakati ambapo marais 3 ECOWAS wakiwasili nchini humo kumuarifu tarehe ya mwisho ya kuondoka madarakani kwa hiyari yake au zitumike nguvu za kijeshi

https://p.dw.com/p/zqh2

Marais hao kutoka Benin, Cape Verde na Siera Leone, ambao tayari wameishawasili, watawasilisha ujumbe wa mataifa hayo ya jumuiya ya ECOWAS, kumtaka Bwana Gbagbo aondoke madarakani ili kusuluhisha mzozo wa kisiasa nchini humo.

Lakini kiongozi huyo wa Cote d´Voire ameonya kwamba kitisho hicho cha ECOWAS kutumia nguvu za kijeshi kumuondoa madarakani kinaweza kuitumbukiza nchi hiyo katika vita.

Mpinzani wake Allassane Ouattara anatambuliwa na jumuiya ya kimataifa kuwa ndiye mshindi halali wa uchaguzi wa mwezi uliopita, lakini Gbagbo ameng´ang´ania madaraka kwa msaada wa jeshi. Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani pia zimelaani hatua hiyo ya Gbagbo.