Maporomoko yaua Zaidi ya 30
26 Desemba 2007Matangazo
TAWANGMANGU
Si chini ya watu 33 wamefariki na wengine 41 hawajulikani waliko kufuatia maporomoko ya matope yaliyosababishwa na mvua kubwa katika kisiwa cha Java nchini Indonesia.
Maporomoko hayo ya matope yametokea leo hii katika maeneo ya Karanganyar na Wonogiri baada ya kunyesha mvua kubwa iliyochukua muda wa saa 12.