1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yaua watu 62 Uganda

27 Novemba 2016

Watu hao wamepoteza maisha kwenye mapigano yaliyozuka Magharibi mwa Uganda baina ya majeshi na wanamgambo wanaotaka kujitenga. Polisi wamemkamata Mfalme wa kabila la Wabakonzo Charles Wesley Mumbere.

https://p.dw.com/p/2TKJC
Uganda Afrika Soldaten Sicherung Demonstration
Picha: picture-alliance/dpa/D.Kurokawa

Wanamgambo wanaaminika kuwa wanamuunga mkono mfalme huyo ambaye ni mkosoaji  mkubwa wa serikali ya Rais Yoweri Museveni. Msemaji wa polisi Andrew Felix Kaweesi amesema polisi 14 na waasi 41 wameuwawa katika mapigano hayo yaliyotokea jana katika mji wa Kasese. Mapigano hayo yalizuka baada ya waasi kuwashambulia wanajeshi waliokuwa wanafanya doria katika mji huo.