1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yapamba moto Yemen

Martin,Prema/ZPR3 Juni 2011

Mapigano makali yanaendelea nchini Yemen, kati ya vikosi vya Rais Ali Abdullah Saleh na wapiganaji wa kikabila wa Sheikh Sadik al-Ahmar, katika mji mkuu Sanaa.

https://p.dw.com/p/RRSM
epa02751127 Yemeni anti-government protesters perform traditional dances during a demonstration demanding the departure of Yemeni President Ali Abdullah Saleh, in Sana'a, Yemen, 25 May 2011. Violent clashes between armed tribesmen and Yemeni security forces continued on 25 May in Sana'a, with mediation efforts abandoned and Yemeni President Ali Abdullah Saleh refusing to step down. Saleh said he would not bow to any foreign pressure and that he would only sign a power-transfer agreement 'in the context of dialogue'. EPA/STRINGER +++(c) dpa - Bildfunk+++
Wapinzani wa serikali ya Rais Ali Abdullah SalehPicha: picture alliance/dpa

Mapigano hayo yamesababisha vifo na hata uwanja wa ndege wa Sanaa kufungwa kwa masaa kadhaa. Wapinzani wa serikali wanaomtaka Rais Saleh kuondoka madarakani, wanaandamana tangu mapema mwaka huu. Hadi sasa, jitahada za nchi za Ghuba kupata maafikiano, hazikufanikiwa na Rais Saleh anaetawala tangu miaka 33 anakataa kuondoka madarakani.