1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yaendelea Sudan licha ya matumaini ya utulivu

30 Juni 2023

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa nchini Sudan licha ya matumaini ya kuwepo utulivu katika siku hizi za sikukuu ya Eid al-Adha.

https://p.dw.com/p/4TGrZ
Sudan Kämpfe
Picha: Stringer/IMAGESLIVE via ZUMA Press Wire/picture alliance

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa nchini Sudan licha ya matumaini ya kuwepo utulivu katika siku hizi za sikukuu ya Eid al-Adha. Jana, mripuko mkubwa umetokea karibu na makao makuu ya Jeshi la Sudan na kusikika kote mjini Khartoum.

Chanzo cha mripuko huo hakikuweza kuthibitishwa mara moja, na hakukuwepo na taarifa za haraka kuhusu majeruhi. Kaskazini magharibi mwa Khartoum, ndege za kivita za jeshi zilianzisha mashambulio ya anga dhidi ya wanajeshi wa RSF.

Vita vya kikatili vilivyoanza Aprili 15 mwaka huu kati ya mkuu wa jeshi, Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani, kamanda wa kikosi cha RSF, Mohamed Hamdan Daglo, vimesababisha vifo vya watu wasiopungua 2,800 huku wengine 645,000 wakilazimika kukimbilia nchi jirani. Kulingana na Umoja wa Mataifa, karibu Wasudan milioni 2.2 zaidi ni wakimbizi wa ndani.