Mapigano Gaza | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mapigano Gaza

Watu wa nne wameripotiwa kuwawa kutokana na ndege za kijeshi za Israel kuendelea kulishambulia eneo la Gaza, ndege hizo zikijibiza mashambulizi ya makombora yanayopigwa na wapiganaji wa kipalastina dhidi ya Israel. Waku wa Israel wanasema wataendelea na mashambulizi yao na ikiitaji hata viongozi wa kundi la Hamas watawafata kwote waliko.

Mshanbulio ya Gaza

Mshanbulio ya Gaza

Ndege za kivita za Israel leo zimeshambulia kwa makombora na kuwawaua wapiganaji wa nne wa kundi la Islamic Jihad na kuliteketeza kabisa gari walilokuemo.Tukio hilo limetokea eneo la Beit Lahiya kaskazini mwa Ghaza. Kabla ya hapo mtu moja aliuwawa katika shambulio hilo Israel ikisema walikilenga kituo kimoja cha kutengenezea makombora na hali wapalastina wakisema kituo hicho ni cha kupasulia mawe.

Jana ndege za Israel zilishambulia nyumba moja ya kiongozi wa Hamas Khalil Al-Hayya na kuwauwa watu wa nane wa familia ya Bw Khalil, lakini yeye mwenyewe Bw Khalil hakujeruhiwa.

Israel imekua ikawasaka wapiganaji wa Hamas katika ukingo wa magharibi na pia kuvifunga vituo vinne vya TV katika mji wa Nablus kua vina shirikiana na kundi la Hamas.

Kamati ya bunge inayohusika na usalama nchini Israel jana ilitoa uamuzi wa kuongeza mashambulizi dhidi yawa palastina ,huku waziri wa miundo mbinu wa Israel, Benjamin Bin Eliezer

akisema wapalastina wanaorusha makombora nchini Israel na wale wanaotoa uamuzi huo wote Israel itawapa kipigo kikubwa .

Waziri wa usalama wa ndani wa Israel, Avi Dichter amesema hata akiwa kiongozi wa Hamas, Khaled Meshaal anaeishi uhamishoni nchini Syria hatosalimika na mashambulizi ya Israel,

na hata akiwa waziri mkuu wa palastina, Ismael Haniyeh, kiongozi wa kundi la Hamas katika palastina, ikisadikika kua amekua akiamrisha Hamas iipige Israel kwa makombora, basi nae hatosalimika na mashambulizi

ya Israel.

Hii itakua mara ya pili Israel kujaribu kumua Khaled Mishaal, kiongozi wa kundi la Hamas, ambapo mwaka 1997 wa Israel walijaribu kumua kiongozi huyo wa Hamas alipokua akiishi uhamishoni nchini Jordan.

Moja ya waku wa Hamas , Mushir Al-Masri amesema mauaji yoyote yatakayo tokea ya viongozi wao, basi watakua wamevuka msitari mwekundu na awamu mpya ya mapigano itakua imeanza.

Tangu ijuma nne iliopita ndege za kivita za Israel zilianza kuwashambulia wapiganaji wa Hamas katika maeneo yawa Palastina, na watu karibu 35 wameuwawa katika mapigano hayo.

Nae Havier Solana mwaakilishi mkuu ,wa siasa ya njee ya Umoja wa ulaya, ataelekea Mashariki ya kati kujaribu kutuliza hali ya mapigano inayo endelea kwenye eneo hilo.

.

Watu wa nne wameripotiwa kuwawa kutokana na ndege za kijeshi za Israel kuendelea kulishambulia eneo la Gaza, ndege hizo zikijibiza mashambulizi ya makombora yanayopigwa na wapiganaji wa kipalastina dhidi ya Israel.

Waku wa Israel wanasema wataendelea na mashambulizi yao na ikiitaji hata viongozi wa kundi la Hamas watawafata kwote waliko.

Ndege za kivita za Israel leo zimeshambulia kwa makombora na kuwawaua wapiganaji wa nne wa kundi la Islamic Jihad na kuliteketeza kabisa gari walilokuemo.Tukio hilo limetokea eneo la Beit Lahiya kaskazini mwa Ghaza. Kabla ya hapo mtu moja aliuwawa katika shambulio hilo Israel ikisema walikilenga kituo kimoja cha kutengenezea makombora na hali wapalastina wakisema kituo hicho ni cha kupasulia mawe.

Jana ndege za Israel zilishambulia nyumba moja ya kiongozi wa Hamas Khalil Al-Hayya na kuwauwa watu wa nane wa familia ya Bw Khalil, lakini yeye mwenyewe Bw Khalil hakujeruhiwa.

Israel imekua ikawasaka wapiganaji wa Hamas katika ukingo wa magharibi na pia kuvifunga vituo vinne vya TV katika mji wa Nablus kua vina shirikiana na kundi la Hamas.

Kamati ya bunge inayohusika na usalama nchini Israel jana ilitoa uamuzi wa kuongeza mashambulizi dhidi yawa palastina ,huku waziri wa miundo mbinu wa Israel, Benjamin Bin Eliezer

akisema wapalastina wanaorusha makombora nchini Israel na wale wanaotoa uamuzi huo wote Israel itawapa kipigo kikubwa .

Waziri wa usalama wa ndani wa Israel, Avi Dichter amesema hata akiwa kiongozi wa Hamas, Khaled Meshaal anaeishi uhamishoni nchini Syria hatosalimika na mashambulizi ya Israel,

na hata akiwa waziri mkuu wa Palastina, Ismael Haniyeh, kiongozi wa kundi la Hamas katika Palastina, ikisadikika kua amekua akiamrisha Hamas iipige Israel kwa makombora, basi nae hatosalimika na mashambulizi

ya Israel.

Hii itakua mara ya pili Israel kujaribu kumua Khaled Mishaal, kiongozi wa kundi la Hamas, ambapo mwaka 1997 wa Israel walijaribu kumua kiongozi huyo wa Hamas alipokua akiishi uhamishoni nchini Jordan.

Moja ya waku wa Hamas , Mushir Al-Masri amesema mauaji yoyote yatakayo tokea ya viongozi wao, basi watakua wamevuka msitari mwekundu na awamu mpya ya mapigano itakua imeanza.

Tangu ijuma nne iliopita ndege za kivita za Israel zilianza kuwashambulia wapiganaji wa Hamas katika maeneo yawa Palastina, na watu karibu 35 wameuwawa katika mapigano hayo.

Nae Havier Solana mwaakilishi mkuu ,wa siasa ya njee ya Umoja wa ulaya, ataelekea Mashariki ya kati kujaribu kutuliza hali ya mapigano inayo endelea kwenye eneo hilo.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com