1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maonyesho ya 63 ya magari na kampeni ya uchaguzi mkuu

Oumilkher Hamidou17 Septemba 2009

Homa ya kampeni ya uchaguzi mkuu yazidi kupanda nchini Ujerumani ambako maonyesho ya kimataifa ya magari yafunguliwa rasmi hii leo

https://p.dw.com/p/Jiho
Walinzi wa mazingira watembeza gari linalofaaPicha: AP

Maonyesho ya kimataifa ya magari mjini Frankfurt am Main, na kuzidi kupanda homa ya kampeni ya uchaguzi mkuu nchini Ujerumani, ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Tuanze lakini na kufunguliwa rasmi hii leo na kansela Angela Merkel maonyesho makubwa kabisa ya kimataifa ya magari katika mji mkuu wa kiuchumi wa Ujerumani Frankfurt Am Main.Magari ya anasa yanaonyeshwa katika maonyesho haya ya 63 licha ya mgogoro wa kiuchumi ambao umeathiri vibaya zaidi sekta ya magari.Kivutio cha maonyesho ya magari ya mwaka huu ni yale magari yanayoendeshwa kwa umeme na yale ya nishati mbadala.Gazeti la Bild Zeitung la mjini Berlin linaandika:

Katika maonyesho haya makubwa kabisa ya kimataifa ya magari,kila mtu anazungumzia kuhusu magari yanayoendeshwa kwa umeme.Kuanzia VW hadi kufikia magari ya Daimler,kuanzia Toyota hadi Renault.Ni habari za kuvutia hizo ,seuze tena eti ni rahisi,masafi,ya kimambo leo na zaidi kuliko yote yanaambatana na kanuni za kuhifadhi hali ya hewa.Hayo hasa ndiyo mnunuzi anayoyataka.Na ilivyokua tuko katika kampeni za uchaguzi,wanasiasa wanafikiria pia uwezekano wa kuwapa zawadi ya fedha wale watakaonunua magari yanayoendeshwa kwa umeme.Ulimwengu mzuri wa magari sio?Hasha tusidanganyike.Magari yanayoendeshwa kwa umeme ni kiini macho tuu cha makampuni ya magari yanayotaka kujitoa kimaso maso kwa kusababisha mazingira kuchafuliwa.Kwasababu makampuni ya magari yamechelewa kufikiria tekonolojia mpya.

Gazeti la NÜRNBERGER ZEITUNG linaandika:

Tusijihadae.Wengi wetu hatutokua hai kuweza kushuhudia magari ya jumla jamala ambayo hayachafui mazingira.Sawa,hapatapita muda magari yanayoendeshwa kwa umeme yataanza kuuzwa madukani-lakini watakayo yanunua ni wale tuu wenye kujimudu kifedha.

Symbolbild Wahlkampf im Internet Wählermobilisierung
Picha moja wapo ya kampeni za uchaguziPicha: dpa

Mada yetu ya pili inahusu kampeni ya uchaguzi mkuu.Siku kumi kabla ya uchaguzi mkuu kuitishwa ,vyama vikuu vinajaribu kupima muungano wa aina gani unabidi kuundwa baada ya September 27.Gazeti la BRAUNSCHWEIGER ZEITUNG linachambua matamshi ya waziri wa fedha wa serikali kuu,Peer Steinbrück wa kutoka chama cha SPD aliyependekeza uendelezwe muungano pamoja na vyama ndugu vya CDU/CSU.Gazeti linaendelea kuanadika:

Waziri wa fedha Steinbrück anajulikana upande huo-anasema ukweli hata kama unaudhi.Shauri lake kutaka serikali ya muungano wa vyama vikuu iendelezwe ni miongoni mwa ukweli huo.Na kusema kweli SPD ina njia gani nyengine ya kuendelea kuwepo madarakani?Wenyewe hawasemi hadharani tuu kwasababu wanahofia wasije wakamharibia mambo mgombea wa kiti cha kansela Frank-Walter Steinemeir.

Gazeti la SÜDKURIER linaandika:

Patashika ni kubwa zaidi kusini mwa Ujerumani ambako vyama ndugu vya CDU/CSU vinaweza kupoteza mengi.Lakini wanataka kumshambulia nani?SPD? Merkel atalazimika kushirikiana nao pindi kura hazitatosha kuunda muungano pamoja na chama cha kiliberali cha FDP. CDU wametangaza wazi kabisa wanapendelea kuunda muungano pamoja na FDP,lakini waziri mkuu wa jimbo la kusini la Bavaria Horst Seehofer wa kutoka chama cha CSU anakitia ila chama hicho kidogo cha manjano.Malumbano yoyote yale yatatishia juhudi za kuunda muungano baada ya uchaguzi.

Mwandishi:Hamidou Oummilkhheir/Dt Zeitungen

Mhariri:M.Abdul-Rahman