1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri.

Abdu Said Mtullya16 Desemba 2010

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanazungumzia juu ya msimamo wa Kansela Merkel juu ya mgogoro wa Euro.

https://p.dw.com/p/QdfD
Bundeskanzlerin Angela Merkel spricht am Dienstag, 10. November 2009, im Bundestag in Berlin. Merkel gab die erste Regierungserklaerung nach ihrer Wiederwahl ab. (AP Photo/Gero Breloer) --- German Chancellor Angela Merkel delivers her speech in the German Federal Parliament in Berlin, on Tuesday, Nov. 10, 2009. Merkel says her new government's top priority is overcoming the effects of the economic crisis _ but she warns they will intensify before the situation improves. (AP Photo/Gero Breloer)Picha: AP

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanazungumzia juu ya msimamo wa Ujerumani kuhusu mgogoro wa Euro, juu ya mageuzi katika jeshi la Ujerumani na juu ya mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya.Kansela wa Ujerumani amefafanua msimamo wa nchi yake juu ya mgogoro wa sarafu ya Euro katika tamko alilitoa bungeni.

Gazeti la Reutlinger General Anzeiger linasema, katika tamko hilo Kansela Merkel alieleza wazi kabisa kwamba atakuwa na msimamo mkali juu ya suala hilo. Na amesema labda ataruhusu vipenyo fulani katika taratibu fulani. Lakini mhariri wa gazeti la Reutlinger General Anzeiger anasema hapo pana tatizo; kwamba vipenyo hivyo vya walakini vimeshakuwa sheria siku nyingi. Jambo muhimu ni kwa Kansela Merkel kuonyesha msimamo wazi juu ya sera za kuleta utengemavu wa sarafu ya Euro. Lazima Kansela Merkel achukue hatua baada ya kukuru kakara za wiki jana zilizosababisha wasiwasi kwenye masoko ya hisa.

Gazeti la Der neue Tag linausifu msimamo huo mkali wa Kansela wa Ujerumani juu ya mgogoro wa Euro .Gazeti hilo linasema ikiwa nchi nyigine zinamwona Kansela Merkel kuwa ni mshika bango la nidhamu ya bajeti, basi hizo ni pongezi kwa kansela.Ni kweli kwamba Ujerumani siyo mfano mzuri wa pekee katika masuala ya bajeti lakini pia ni kweli kwamba wajerumani hawaishi nje ya uwezo wao kwa kiwango kinachofanyika katika nchi nyingine. Kwa hiyo hakuna nchi mwanachama wa Umoja wa sarafu ya Euro mwenye haki ya kuwa kupe na kuwanyonya damu wengine .Kila nchi inapaswa kuwa na nidhamu katika matumizi.

Gazeti la Nürnberger lina wasiwasi juu ya msimamo wa Kansela Merkel katika ngazi ya kimataifa na hasa leo ambapo viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels.

Mhariri wa gazeti hilo anayatilia maanani madai yaliyotolewa na waziri wa fedha wa Luxemburg Juncker kwamba msimamo wa Kansela Merkel unaenda kinyume na malengo ya Umoja wa Ulaya.Mhariri huyo anasema madai hayo yanaweza kuiletea madhara Ujerumani.

Gazeti la Hannoversche Allgemeine linatoa maoni juu ya mageuzi yaliyofanywa katika jeshi la Ujerumani.Linasema pana maswali mengi yanayopaswa kujibiwa na waziri wa ulinzi.Mojawapo ni,jee baada ya kubana matumizi, vipi Ujerumani itautekeleza wajibu wake katika mifungamano na nchi nyingine duniani?

Mwandishi/Mtullya Abdu/

Deutsche Zeitungen

Mhariri/ Josephat Charo