1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini.

Abdu Said Mtullya7 Mei 2009

Magazeti ya Ujerumani leo yanazungumzia juu ya mkataba wa Lisbon na juu ya mazoezi ya kijeshi ya nchi za NATO.

https://p.dw.com/p/HlZn
Majeshsi ya Nato yanaendelea na mazoezi ya kijeshi nchini Georgia.Picha: AP

Wahariri  wa  magazeti ya Ujerumani leo wanatoa maoni yao  juu  ya mkataba mpya wa Umoja  wa Ulaya  na juu ya mazoezi ya kijeshi  yanayofanywa  na nchi za Nato  nchini  Georgia .

Mkataba wa Umoja  wa Ulaya-unaoitwa mkataba  wa Lisbon unapaswa kuidhinishwa  na  nchi  zote  wanachama wa Umoja  huo ili uweze kutumika. Lakini   pamekuwa  na  mashaka mashaka miongoni  mwa  wanachama fulani.

Hatahivyo  gazeti  la  Darmstädter  Echo linasema  Umoja  wa  Ulaya ungali hai!

Mhariri wa  gazeti hilo  anasema  katika maoni yake kwamba  Umoja  wa  Ulaya bado ungali hai-  kwa  sababu  bunge la nchi  Jamhuri  ya Czech  limeukubali mkataba  huo  wa mageuzi.

Mhariri  huyo  anatilia  maanani  kwamba Jamhuri  ya  Czech iilikuwa miongoni mwa nchi  zilizokuwa  zinayumbayumba kuhusu mkataba  huo.

Na mhariri  wa  gazeti la Münchner Merkur anasema  hatua  ya seneti ya Jamhuri  ya Czech kuukubali na kuupitisha  mkataba  huo angalau katika seneti, ni  ishara ya  matumaini.

Gazeti  hilo linasema licha  ya kasoro na maswali mengi yaliyopo juu  ya mkataba wa Lisbon, uamuzi wa seneti ya Jamhuri   ya Czech  umekuja  wakati mujarab-kwani  ni  hatua inayoashiria kuondokana na  taasisi zinazojikwamishwa  zenyewe  ndani  ya Umoja wa Ulaya. Gazeti la Münchner Merkur linatilia  maanani kwamba wananchi zaidi  na  zaidi katika  nchi  za Umoja  wa Ulaya  wanatambua umuhimu wa bara  lao katika kuwa  na uwezo  wa  kuchukua hatua, kama jinsi inavyoonekana  sasa katika nyakati  za mgogoro wa  uchumi unaoikabili  dunia.


Gazeti  la Financial  Times Deutschland pia  linazungumzia  juu  ya  mkataba   wa Lisbon  kwa  kuipongeza  Jamhuri  ya Czech  kwa hatua  iliyochukua ili kulisogeza  mbele  bara  la Ulaya.


Gazeti  la  Westdeutsche Zeitung linazungumzia juu ya mazoezi  ya  kijeshi ya nchi  za  Nato nchini  Georgia.

Mhariri  wa  gazeti hilo  anasema kuwa licha ya upinzani na shutuma za Urusi mazoezi hayo yaliyoanza  jana  nchini Georgia, lazima yaendelee  kufanyika la sivyo  Nato  itavurugika wajihi.