1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nishati ya nyuklia kuendelezwa Ulaya

Admin.WagnerD18 Mei 2016

Wahariri wanatoa maoni juu ya mkakati wa Umoja wa Ulaya kihusu nishati ya nyuklia na pia wanasema madhali uroho wa fedha unaendelea, madawa ya kuongeza nguvu pia yataendelea kutumiwa katika michezo

https://p.dw.com/p/1IpmF
Kinu cha nyuklia nchini Ujerumani chini ya maji
Kinu cha nyuklia nchini Ujerumani chini ya majiPicha: picture-alliance/dpa/I. Wagner

Gazeti la "Volkssstimme" linautilia maanani mkakati wa Umoja wa Ulaya kuhusu nishati ya nyuklia. Umoja huo unatarajia kuchapisha mtaala juu ya nishati hiyo.

Mhariri wa gazeti hilo anasema inapasa kutambua ukweli kwamba katika nchi nyingi za Umoja wa Ulaya ipo mipango ya kuendeleza matumizi ya nishati ya nyuklia au ipo mipango ya kuinua viwango vya ugavi wa nishati hiyo ili vitimize mahitaji ya sasa.

Mhariri wa "Volksstimme" anatilia maanani kwamba mkakati wa Umoja wa Ulaya juu ya nishati ya nyuklia unapingwa na Ujerumani.Lakini anakumbusha kwamba bado vinu vya nyuklia vipo nchini Ujerumani.

Naye mhariri wa "Allgemeine Zeitung" anasema vinu vya nyuklia vipo katika nchi nyingi, na vitaendelea kuwepo, kwa sababu hiyo ndiyo njia ya kujihakikishia mapato.

Duterte ataka adhabu ya kifo Ufilipino

Gazeti la Neue Osnabrücker linazungumzia juu ya mpango wa Rais mteule wa Ufilipino ,Duterte wa kuirejesha adhabu ya kifo.

Rais mteule wa Ufilipino Rodrigo Duterte
Rais mteule wa Ufilipino Rodrigo DutertePicha: Reuters/E. de Castro

Linasema kabla ya uchaguzi Duterte alitangaza mpango juu ya kuwanyonga maalfu ya wahalifu. Sasa baada ya miaka 10 kupita Raisi mteule huyo anataka kurudisha adhabu ya kifo. Gazeti linasema kwa jumla mipango ya bwana Duterte inaenda kinyume siyo tu na utawala wa kisheria bali pia na maadili ya kibinadamu.

Hata hivyo mhariri wa gazeti la "Neue Osnabrücker" anatilia maanani kwamba bwana Duterte anaungwa mkono na wapiga kura licha ya sera zake .Mhariri huyo anaeleza kuwa hayo yanaonyesha ni kwa kiasi gani watu wamevunjika nyoyo nchini Ufilipino hadi kufikia hatua ya kumpa ukumbi mwanasiasa kama huyo.

Vita dhidi ya dawa za kuongeza nguvu katika michezo havitafanikiwa

Gazeti la "Rheinpfalz" linazungumzia juu ya madai ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu yanayoelekezwa kwa wanamichezo ya Urusi.

Mhariri wa gazeti hilo anasema madhali watu fulani wapo tayari kutoa fedha ili kutangaza biashara zao,kwa njia ya kuwatumia wanamichezo, uovu wa matumizi ya dawa hizo, hautakomeshwa duniani. Watu hao wanajaribu kuwafanya watu wengine waamini yale ambayo si kweli, kuwa kweli.

Mwandishi:Mtullya Abdu,/Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman