Magazetini.
17 Desemba 2008Pia wanazungumzia juu ya malengo ya rais mteule wa Marekani, Barack Obama.
Na magazeti ya Volksstimme na Neue Osnabrücker yanatathmini yaliyotekelezwa na rais Sarkozy wa Ufaransa katika kipindi cha miezi sita iliyopita ambapo aliuongoza Umoja wa Ulaya.
Juu ya Afrika ya Kusini gazeti la Berliner Zeitung linasema kuzinduliwa chama kipya cha kisiasa nchini kunatoa fursa ya mashindano ya maoni ya kisiasa. Gazeti linasema kuundwa chama kipya cha kisiasa nchini Afrika kusini ni fursa kwa wapiga kura ya kutafuta njia mbadala nchini humo .
Gazeti linasema hiyo ni changamoto kubwa kwa chama kinachotawala sasa-ANC.
Gazeti la Berliner Morgenpost linazumngumzia rais mteule wa Marekani Barack Obama.
Linasema Obama anaonekana kama rais wa dunia nzima, lakini hali halisi, imo ndani ya nchi yake.
Mhariri wa gazeti la Berliner Morgenpost anaeleza kuwa jambo la kipaumbele kwa Obama sasa ni kuimarisha mamlaka yake ndani ya Marekani. Mtihani wake wa kwanza utakuwa mnamo mwaka wa 2010 ambapo uchaguzi wa bunge utafanyika. Gazeti linatilia maanani lengo la Obama juu ya kuhakikisha wingi wa wajumbe wa chama cha Demokratik kwenye seneti na kwenye baraza la wawakilishi.
Gazeti la Schwäbische Zeitung pia linazungumzia juu ya dhamira ya rais meteule Obama juu ya kuleta sera mpya katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Gazeti hilo linasema dhamira ya Obama imethibitika katika uteuzi wa waziri mpya wa nishati Steven Chu. Mhaariri wa Schwäbische Zeitung anaeleza kuwa kuteuliwa kwa waziri huyo mpya bwana Chu kunaimarisha matumaini juu ya dhamira ya rais mteule Barack Obama katika kukabiliana na janga la mabadiliko ya hali ya hewa. Gazeti linatilia maanani kuwa waziri Chu ni mtetezi wa mabadiliko yanayokusudiwa kuletwa na Barack Obama.Lakini hayo yataonekana kwenye mkutano wa kilele juu ya hali ya hewa utakaofanyika mjini Kopenhagen mwaka ujao.