1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo

Josephat Charo22 Agosti 2007

Kufutia kisa cha Wahindi kushambuliwa mjini Mügeln katika jimbo la Sachsen hapa Ujerumani, mjadala kuhusu uhasama dhidi ya wageni bado unaendelea.

https://p.dw.com/p/CHS4

Mhariri wa gazeti la Süddeutsche anasema kiwango cha uadui dhidi ya wageni na kusambaa mawazo ya kiimla kunapungua kupitia maendeleo, elimu, maendeleo binafsi ya kitabia na kama ufanisi unavyoonyesha wengi wanazungumzia juu ya uthabiti wa jamii na demokrasia. Je jimbo na kuwa na fedha nyingi kunatakiwa kuwa na thamani kubwa.

Mhariri wa gazeti Süddeutsche anasema kinachotakiwa kupigwa vita duniani ni uhasama dhidi ya wageni lakini hilo halifanyiki. Na hapa Ujerumani ukweli huo unaumiza, sio kwa sababu Wajeruamani ni maadui wakubwa wa wageni kuliko wazungu wengine ila nchini Ujerumani uhasama dhidi ya wageni umeshawahi wakati mmoja kuwa kama imani ya jimbo.

Gazeti la Handelsblatt la mjini Düsseldorf linasema anayedunisha shambulio dhidi ya Wahindi katika mji wa Mügeln mashariki mwa Ujerumani kuwa tatizo lenye mpaka, anakosa kutathmini athari zinazoweza kutokea katika ngazi ya kimataifa. Kwa kuwa Ujerumani inapitia wakati ambapo uchumi wake unaimarika na inakabiliwa na upungufu wa wataalamu, hali hiyo inawafungulia mlango wasomi wa kigeni kutoka India walio na ujuzi kupata ajira zenye mishahara mizuri, ambazo ni nadra kuchapishwa katika magazeti ya nchi za kigeni.

Lakini picha ya Kulvir Singh, mhindi aliyemiliki mkahawa mjini Mügeln, ilichapishwa kwenye kurasa za mwanzo za magazeti nchini India, huku bwana huyo akionekana akitokwa na damu baada ya kipigo alichokipata kutoka kwa Wajerumani wanaowachukia wageni. Gazeti la Hindustan Times kwa mfano lilikuwa na kichwa cha habari kilichosema, ´Shambulio la ubaguzi wa rangi nchini Ujerumani.´ Taarifa hiyo itabakia katika kumbukumbu.

Gazeti la Kölnischer Rundschau linasema shambulio dhidi ya Wahindi mjini Mägeln ni aibu! Ni aibu pia jinsi watu walivyolichukulia shambulio hilo! Hawa ni binadamu waliowindwa, kupigwa na kusukumwa katika hofu ya kifo. Ukatili huo umezusha mjadala juu ya swala ikiwa wavamizi ni washambuliaji wa kihafidhina au ni watu wanaowachukia tu wageni.

Kana kwamba hilo ndilo tatizo linalotakiwa kushughulikiwa kwa haraka, je ni picha gani inayoonyesha mji huo mdogo wa jimbo la Sachsen kutokana na washambuliaji wa kijerumani kuwapiga raia wa kihindi.

Nalo gazeti la Landeszeitung kutoka mjini Lüneburg limeandika: Hatua ya watu kuhofu kimya kimya kwamba maadili ya kijamii yanaporomoka, inawapa nguvu washambuliaji. Hali ya kutojali tukio la kupigwa kwa Wahindi mjini Mügeln inaonyesha ni kwa umbali gani manazi mamboleo walivyofaulu kuligeuza jimbo hilo la mashariki wa Ujrumani kuwa la mafashisti.

Naye mhariri wa gazeti la Stuttgarter akizungumzia shambulio dhidi ya Wahindi amesema ni mwiko magharibi mwa Ujerumani, lakini katika eneo la mashariki demokrasia sasa inatiliwa shaka. Mtu hakumbuki tu hisia mbaya alizopata katika mji huo. Kwa mifumo mingi, demokrasia ni chombo kinachowawezesha wengi kujipatia nafasi katika maisha. Huo ndio msingi mzuri wa kuhakikisha haki zote zinaheshimiwa.

Sera iliyopo mpaka leo inasema raia watabeba dhamana iwapo hawataheshimu demokrasia. Mhariri anamalizia kwa kusema hilo ndilo walifanyalo Wajerumani wanaonyamaa kimya na kutazama yanayoendelea kama vile wakaazi wa Mügeln.