1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya mauaji ya Munic

Wahariri wa magazeti wanazungmzia juu ya maafa yaliyotokea miaka 40 iliyopita mjini Munic, kwenye michezo ya Olimpiki, ambapo magaidi waliwaua Waisraeli 11

Kumbukumbu ya mauaji ya wanamichezo wa Israel mjini Munic mwaka 1972

Kumbukumbu ya mauaji ya wanamichezo wa Israel mjini Munic mwaka 1972

Gazeti la" Badische" linakumbusha juu ya sera ya nje ya Ujerumani kuhusu Israel baada ya kutokea maangamizi ya Wayahudi-Holocaust. Jee Mjerumani anapaswa kuhusiana vipi na Israel baada ya maangamizi yaliyofanywa na Hitler na pia vipi Ujerumani inapaswa kuhusiana na Wapalestina na nchi za Kiarabu?

Mhariri wa gazeti la "Badische" anasema maswali hayo yanaonyesha jinsi wahusika wa usalama walivyohamanika baada ya wanamichezo wa Israel kuuliwa na magaidi kwenye michezo ya Olimpiki mjini Munic miaka 40 iliyopita.


Mhariri wa gazeti la "Neue Ruhr/Neue Rhein" pia anatoa maoni juu ya mkasa huo wa miaka 40 iliyopita, kwa kutulia maanani yale yanayotokea kila siku nchini Ujerumani-yaani chuki dhidi ya wayahudi. Mhariri huyo anasema maswali mengi yaliyoulizwa juu ya kushindikana kwa juhudi za kuwakomboa wanamichezo wa Israel waliotekwa nyara wakati wa michezo ya olimpiki miaka 40 iliyopita ndio ulikuwa msingi wa kuundwa kwa kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi nchini Ujerumani,GSG 9. Mauaji yaliyofanywa na magaidi kwenye michezo ya mjini Munic yalikuwa ishara ya kumea kwa kundi la magaidi wa Ujerumani-"RAF."

Gazeti hilo linasema ukweli wa kusikitisha juu ya Ujerumani ni kwamba hadi katika mwaka huu wa 2012 vitendo vya kutumia nguvu dhidi ya wayahudi bado vinaendelea kutokea nchini.

Gazeti la "Lübecker Nachrichten" linauzungumzia mgogoro wa Syria kwa kulitilia maanani tatizo la wakimbizi wa nchi hiyo. Mhariri wa gazeti hilo anasisitiza katika maoni yake kwamba wanaopaswa kusaidiwa ni wale wasiokuwa hatia.

Gazeti hilo linasema muhimu ni kuwasaidia wananchi wa Syria wanaotumbukia katika matatizo bila ya kuwa na hatia. Msaada huo unaweza kutolewa katika nchi ambazo ni jirani wa Syria kama ambavyo Ujerumani inafanya. Lakini inawezekana kuwasaidia wakimbizi pia ndani ya Syria kwenyewe, mradi inatengwa sehemu ya kuwalinda wakimbizi hao chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa, bila ya kuwapeleka walinzi wenye silaha. Madhali Ujerumani sasa itakuwa Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa muda wa mwezi mmoja,hiyo itakuwa fursa nzuri ya kuwasilisha pendekezo kwenye Baraza hilo.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen/

Mhariri:Yusuf Saumu