1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya Afrika ya Kati

Abdu Said Mtullya21 Januari 2014

Wahariri wa magazeti wanazungumzia juu ya mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mvutano wa kisiasa nchini Ukraine na juu ya kukaribiana kwa Iran na nchi za magharibi

https://p.dw.com/p/1AuAS
Rais wa kipindi cha mpito ,katika Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba Panza
Rais wa kipindi cha mpito ,katika Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba PanzaPicha: Reuters

Gazeti la "Nürnberger Nachrichten" linazitahadharisha nchi za Umoja wa Ulaya juu ya mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati . Mhariri wa gazeti hilo anasema Umoja wa Ulaya unataka kujiingiza katika mgogoro huo bila ya kuwa na mpango maalumu. Mhariri huyo anasema matokeo yake yatakuwa kurukaruka kati ya migogoro.

Lakini Mhariri wa gazeti la "Saarbrücker" anaifafanua sababu ya nchi za Umoja wa Ulaya kujiingiza katika mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Anasema ikiwa nchi za kaskazini mwa Afrika zitavurugika, athari zake zifafika hadi barani Ulaya. Ndiyo kusema Ujerumani pia itakumbwa na athari hizo.Na kwa hivyo kutokana na kuwa taifa kubwa la kiuchumji duniani Ujerumani haiwezi kuyapuuza yanayotokea katika bara jirani.

Gazeti la "Badische" pia linauzungumzia uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kusaidia katika juhudi za kuutatua mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.Lakini mhariri wa gazeti hilo anasema Umoja wa Ulaya unahitaji kuwa na mpango maalumu.

Mvutano nchini Ukraine

Na sasa tugeukie katika mvutano wa kisiasa wa nchini Ukraine.Ni muda mrefu sasa tokea mvutano huo uanze katika nchi hiyo.Na hakuna dalili za kumalizika. Mhariri wa gazeti la "Badische Neuste Nachrichten" anasema hatari ya kumwagika damu ni kubwa nchini Ukraine.

Sasa Umoja wa Ulaya hauna budi ufanye kila litakalowezekana kuwaleta pamoja wapinzani na wawakilishi wa serikali ili wafanye mazungumzo. Iwapo juhudi hizo zitafanikiwa au la ni jambo jngine.Lakini muhimu ni kujaribu. Hali nchini Ukraine imekuwa ngumu kiasi kwamba serikali inaweza kupandisha mbogo na kuanza kutumia mabavu ili kuwadhibiti wapinzani.

Iran na nchi za magharibi zakaribiana?

Nchi za magharibi na Iran zimeonyesha dalili za kukaribiana kutokana na juhudi za kidiplomasia zilizochukuliwa, na zinazoendelea kuchukuliwa.Hata hivyo katika maoni yake mhariri wa gazeti la "Nordwest " anasema bado pana uwezekano wa kuwapo tuhuma juu ya mipango ya Iran.

Mhariri huyo anaeleza kwamba nchi za magharibi zimepiga hatua ndogo katika kulifikia lengo lao kuhusiana na Iran.Nchi hizo zinaitaka Iran iachane na mpango wake wa kuyarutubisha madini ya uran. Na hakika Iran imesema kuwa imepunguza kiwango cha kuyarutubisha madini hayo.

Lakini mhariri huyo anasema bado pana haja ya kuwa macho. Sababu ni kwamba itikadi za msingi za Iran bado hazijabadilika. Awali ya yote watawala wa nchi hiyo wanaendelea kuwa wakandamizaji.

Mwandishi:Mtullya Abdu.Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman