1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Maoni: Afrika ya Obama ni uwanja mpana

Kumalizikia nchini Tanzania kwa ziara ya Rais Obama barani Afrika kunaweza kuzingatiwa kuwa ni hatua ya maridhiano. Hata hivyo bara la Afrika bado lipo kandoni mwa ajenda ya Marekani, anasema Claus Stäcker.

Kumalizikia nchini Tanzania  kwa ziara  ya Rais Obama barani Afrika kunaweza kuzingatiwa kuwa ni hatua ya maridhiano. Hata hivyo bara  la Afrika bado  lipo  kandoni mwa ajenda  ya   Marekani.

Mkuu wa idara ya Afrika ya DW, Claus Stäcker.

Mkuu wa idara ya Afrika ya DW, Claus Stäcker.

Maalfu ya watu waliokuwa na furaha   walimlaki Rais Obama  nchini Tanzania. Kituo cha mwisho cha ziara yake  ya barani Afrika kinachoweza kuzingatiwa  kuwa  ni hatua  ya  maridhiano. Huku akishangaliwa sana, Obama alitangaza  alichokiita  kuwa  zama  mpya  za uhusiano  na  bara la Afrika.   Msingi  wa muundo  huo  mpya wa  uhusiano, siyo tena  misaada  ya maendeleo na kuungwa  mkono, bali  uhusiano biashara  na ushirikiano.

Dhima ya Marekani katika uhusiano mpya

Rais Obama amesema  dhima  ya   Marekani hapo itakuwa  ile  ya  mshirika. Hayo ni maneno  mazito yaliyotoka kwa urahisi kwenye kinywa  cha  Obama, Rais wa kwanza  wa  Marekani, mwenye  nasaba  ya Afrika.

Mpango huo siyo  wa kuliwaza sana,kiasi cha kuweza kumweka   Obama katika safu moja na  marais  wa Marekani wa  hapo  awali, Bill Clinton na George  Bush.Wote wawili wameingia katika historia  kutokana na mipango waliyoitekeleza kwa manufaa ya bara la Afrika.

Bill Clinton alitia saini mkataba  wa    Agoa wa  kuzipa fursa nchi  za  Afrika  ya kuuza  bidhaa  nchini  Marekani   bila  ya kutozwa ushuru. Ni mradi  ambao ungeliweza  kuipeleka   Afrika mbali, laiti  ungelitekelezwa kwa makini  zaidi. Bush aliyamimina mabilioni ya fedha barani Afrika kwa  ajili ya mradi wa kuwasaidia  waathirika  wa maradhi ya ukimwi .

Je, itahimili kishindo cha China?

Obama ametangaza kuwa Waziri wake   mpya Penny Pritzer atashughulikia biashara  baina ya  Marekani na  Afrika. Ni kweli kwamba thamani ya biashara kati ya Afrika na Marekani mnamo kipindi  chama  miaka 10 iliyopita iliongezeka mara mbili. Lakini biashara  baina  ya China  na nchi za  Afrika iliongezeka  mara  20 katika  kipindi hicho hicho.

Ni muda mrefu tokea China ilipoichukua nafasi ya Marekani kama  mshirika mkubwa kabisa wa  biashara  na nchi  za Afrika. Tuchukue  mfano wa Tanzania. Biashara  kati ya  nchi hiyo  na Marekani ilifikia thamani  ya  dola Milioni 360 katika mwaka uliopita. Lakini  biashara baina  ya Tanzania na China ilifikia thamani  ya dola  bilioni 2 na nusu.

Wakati Obama, katika muhula wake  wa  pili  wa  urais, alipoamua  kufanya ziara barani Afrika,  viongozi  wa  ngazi   za juu  wa  China siku nyingi walikuwa tayari wameshalitembelea  bara hilo. Rais mpya  wa  China  Xi Jinping alikuwako nchini Tanzania mnamo  mwezi wa Machi. Na kwa hivyo mambo hayatakuwa rahisi kwa waziri mpya  wa biashara   wa Marekani,Penny Pritzer kuitekeleza  ndoto ya Obama juu ya Afrika. 

Nguvu Afrika kubadilisha hali ya mambo?

Hata hivyo kijogoo kinaweza  kuwika kutokana na mpango wa Marekani   wa dola bilioni saba  wa  ugavi wa nishati  ya umeme  kwa  nchi  za Afrika unaoitwa "Nguvu  Afrika." Lengo  lake ni kuongeza ugavi wa umeme mara mbili kwa nchi  za  Afrika  za kusini  mwa  jangwa  la  Sahara . Theluthi  mbili ya watu  wa eneo  hilo  hawapati huduma ya  umeme. Na   nchi sita ikiwa pamoja  na Tanzania  zimo katika hatua  za mwanzo za  kuunganishwa. Kaya milioni 20 zitaunganishwa  katika mtandao wa huduma  hiyo  ya umeme.

Katika  kituo cha kwanza,cha  yake, nchini  Senegal, Obama  bado alikuwamo  mnamo mkondo sahihi,   angalau  mwanzoni. Alienda kwenye kituo kilichotumika  kwa  ajili ya kuwasafirishia  watumwa ng'ambo katika kisiwa cha Goree. Lakini Obama alivuruga mambo aliposositiza juu ya haki za  mashoga  alipozungumza kwenye  mkutano na waandishi  wa habari  na mwenyeji wake Rais Macky  Sall  wa  Senegal.

Lakini  Obama  alijibiwa  na mwenyeji   wake  kwa kwamba hakuna chuki dhidi ya mashoga  nchini Senegal, lakini  nchi  hiyo bado haijawa  tayari  kuepusha kubaguliwa  kwa watu  hao. Ziara  ya Obama , barani  Afrika  ilimalizika  nchini Tanzania, kwa  upeo wa  chini  kama  iliyvoanza  kwa  Rais  huyo  nchini Senegal.