Manila. Upigaji kura waendelea. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Manila. Upigaji kura waendelea.

Upigaji kura unaendelea katika uchaguzi wa muda wa kati nchini Philippines. Kiasi cha watu milioni 45 wanahaki ya kupiga kura.

Upigaji kura umeingia doa kutokana na vifo vya watu sita kutokana na ghasia zinazohusiana na uchaguzi nchini kote.

Zaidi ya watu 120 wameuwawa tangu kampeni za uchaguzi zianze miezi mitatu iliyopita.

Rais Gloria Macapagal Arroyo ana lengo la kuimarisha wingi wa wabunge kutoka chama chake katika bunge la nchi hiyo.

Majeshi ya usalama yamewekwa katika tahadhari ya juu kabisa ili kuzuwia wapiganaji wa chini kwa chini wa kikomunist wanaotaka kuchafua uchaguzi huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com