MANILA: Kiongozi Mkuu wa Kundi la wanamgambo la Abu Sayyaf auawa nchini Philippines. | Habari za Ulimwengu | DW | 20.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MANILA: Kiongozi Mkuu wa Kundi la wanamgambo la Abu Sayyaf auawa nchini Philippines.

Serikali ya Philippines imethibitisha kwamba kiongozi mkuu wa kundi la wanamgambo wa Abu Sayyaf amefariki dunia.

Msemaji wa serikali amesema uchunguzi uliofanywa na Wamarekani wa maiti iliyopatikana mwezi uliopita ulithibitisha kwamba maiti hiyo ni ya Khaddafy Janjalani ambaye zawadi ya dola milioni tano ilikuwa imetangazwa kwa kukamatwa kwake.

Khaddafy Janjalani aliuawa mwezi Septemba mwaka uliopita baada ya mapambano kati ya majeshi na wanamgambo.

Habari za kifo cha kiongozi huyo wa wanamgambo zimetolewa siku chache baada ya kuuawa kiongozi mwengine wa Abu Sayyaf, Abu Sulaiman katika kisiwa cha Joho.

Kundi hilo la Abu Sayyaf linasemekana kuwa na uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com